
Aliyekuwa Naibu wa rais Rigathi Gachagua ameenda 'LIVE' kwenye mtandao wa Tik Tok.
Gachagua alitumia zaidi ya masaa mawili kuzungumuza na wakenya walioungana naye kwenye mtandao. Maelifu ya watumiaje wa mtandao wa Tik Tok walijumuika kumusikiliza.
Gachagua alitumia nafasi hio kuzungumzia maswala kadhaa, likiwemo swala la bima ya afia 'SHA'. pamoja na msitakabali wa kisiasa katika taifa.
Njama ya Gachsgua kutumia mtandao huu inabainisha nia yake ya kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa vijana ambao ndio wengi katika mtando huo na pia kuwafikia wakenya ambao wanaishi ya nchi.
Gachagua hata hivyo amekumbana na changamoto, ikiwa pamoja na sauti kupotea, na kutowafikia wasikilizaji wake kwa njia nzuri.
Naibu wa rais wa zamani ameelekeza lawama kwa serikali na watu wa ujasusi kutokana na shinda iliyotokea katika mtandao alipokua akizungumza na wakenya. Ametaja changamoto hii kwamba, kikosi chake kilikumbana nayo wakati juhudi za kumuondoa mamlakani zilikua zikiendelea.
Gachagua alitumia nafasi hio kulaumu rais Ruto akitaka abebe msalaba wake sababu alishaharibu uhusiano wake na watu wa mlima Kenya na hilo haliwezibadilika.
"Usaliti katika mlima Kenya hauwezi sameheka, limeshatendeka na haliwezi rekebishwa. Hata ukiteuwa mawaziri wote kutoka mlima Kenya hakuna la kubadilika.Hata ungeamsha Dedani Kimathi, Mwai Kibaki au Jomoo Kenyatta. mlimaa umeenda na umeenda," alisema Gachagua.
"Nimeona rais William Ruto akichukua siku tano zote huko magharibi akijadili jina langu, kuliko kuangazia mambo yanayowakumba watu wa eneo hilo. kwani Gachagua ndio shida za watu huko, kwani jina langu ni njia huko Vihiga au pump ya maji Kakamega," Ruto alisema akiwaelekezea viongozi wa serikali ya Kenya kwanza.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!