Gavana wa kaunti ya Busia Paul Otuoma amewaomba wenyeji wa eneo hilo kusimama na serikali ya rais William Ruto.

Otuoma amewataka wenyeji kurejesha mkono kwa sababu rais Ruto atampigia Raila kura katika lengo lake la kuwania nafasi ya kuwa mwenyekiti wa umoja wa Africa.

Kaunti ya Busia ni mojawapo ya ngome muhimu zenye wafwasi wa Raila. Waziri mkuu huyo wa zamani amekuwa akivuna pakukbwa katika chaguzi zote alizojaribu kuwania urais kutokana na wafwasi wengi alionao katika enoe hilo.

Gavana Otuoma amewakumbusha wananchi wa Busia kwamba kura ya Ruto ndio itakayohitajika pekee katika Taifa la Kenya wakati wa uchaguzi huo wa umoja wa Afrika.

"Kama Ruto rais anapigia Agwambo kura, mbona sisi tusirejeshe mkono. Hakuna mtu atatoka kenya kwenda Adis Ababa kupiga kura ispokuwa  Ruto, sisi wengine tutaenda huko kusherekea tu lakini si kupiga kura," alisema Paul  Otuoma.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Otuoma alikua anazungumza haya alipokua ameandamana na rais katika safari yake ya kuzuru magharibi mwa Kenya. Rais William Ruto na viongozi kadhaa wa serikali ya Kenya kwanza wamekua wakizuru kaunti ya Busia Leo Jumanne 22.

Hata hivyo amemtaka rais pia kuweka mipango itakayoinua uchumi wa eneo hilo hasa kupitia kilimo .

Gavana huyo wa pili katika kaunti ya Busia amekuwa mwanachama wa ODM kwa muda mrefu  na mwandani wa Raila tangu akiwa mwakilishi wa eneobunge la Funyula.

Kwa sasa uhusiano wake na rais William Ruto umeongezeka sana. Wiki jana aliwaongoza wabunge wote kutoka kaunti ya Busia kukutana na rais katika ikulu ya Nairobi.