MWANAMKE mmoja amewazuzua watumizi wa mitandao ya kijamii baada ya kufichua kile alichokiita habari njema kwake.
Mrembo huyo alichukua furaha yake kwenye mitandao wa TikTok na kuwafichulia mashabiki wake kwamba hatimaye amepata nafasi katika chuo kimoja kikuu ya kusomea taaluma ambayo amekuwa akitamani.
Mwanamke huyo alisema kwamba kwa muda mrefu, ilikuwa ni ndoto yake kusomea fani ya jinsi ya kutunza maiti na sajili nzima ya mazingira ya makafani.
Alisema kwamba baada ya kutuma maombi, hatimaye chuo kikuu kimoja kilikubali kumchukua na kumpa mafunzo hayo katika kitivo hicho ambacho hakiwavutii wanafunzi wengi.
Katika video hiyo, alionyesha uso wake na nukuu iliyowaacha wengi kushangaa. Aliandika: "Nimekubaliwa katika shule ya ndoto yangu."
Klipu hiyo ilipocheza, ilionyesha arifa ya uandikishaji kwenye simu yake, ikithibitisha kozi hiyo isiyo wa kawaida.
Chapisho hili lilipata umaarufu mtandaoni kwa haraka, na kuibua hisia nyingi kutoka kwa watu waliohusika ambao walikwenda kwenye sehemu ya maoni ili kushiriki mawazo yao.
INNOCENT ❤️?☠️?: “Mafunzo ya Sayansi ya chumba cha maiti ni kozi nzuri sana Yo Yo natania ?. Hakuna idara hii shule yangu haipati ??."
ELYON♠️??♌: "kipi kitakuwa sayansi ya kuhifadhi maiti ??."
Nchini Kenya, miaka miwili iliyopita, chuo anuwai cha mafunzo ya uuguzi, KMTC kilitangaza kuanzishwa kwa kozi ya Wahudumu wa mochari.
“Ulituuliza, tukakusikiliza! Chuo sasa kitakuwa kikitoa Diploma ya Sayansi ya Maiti kuanzia Machi 2023. Ni kozi ya kwanza kabisa katika Afrika Mashariki na Kati.”
“Mafunzo hayo huchukua muda wa miaka 3, huku wale ambao tayari wana cheti katika kozi moja kutoka taasisi nyingine zinazotambulika watajiunga na kozi ya uboreshaji ambayo huchukua miaka miwili. Kwa wanafunzi wa shule ya awali, alama ya wastani ya C- katika KCSE inahitajika huku Cheti cha Sayansi ya Hifadhi ya Maiti ni sharti kwa wanafunzi walio kazini,” KMTC walitangaza kupitia ukurasa wao wa Facebook Januari 2023.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!