KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Januari 22.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Nairobi, Nandi, Uasin Gishu, Nyeri, Embu, Kirinyaga, Bungoma, Kiambu, Mombasa, na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la Githurai 45 zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Keben na Mogobich katika kaunti ya Nandi yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Maeneo ya Cheptiret, Bayete, Lorian, Kerita, Kesses, na Cheptiret katika kaunti ya Uasin Gishu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Mathaithi, Tumutumu Hospital, Milimani na Gatuamba katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Ishiara na Kanyuambora katika kaunti ya Embu yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Ngurubani na Gathigiriri katika kaunti ya Kirinyaga yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Pwani na Nyange katika kaunti ya Bungoma yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ya Kagwe na Kamburu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Jomvu katika kaunti ya Mombasa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Watamu na Gede katika kaunti ya Kilifi pia zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.