
Mwanasiasa George Wajackoyah sasa anasema kwamba aliyekuwa naibu wa rais, Rigathi Gachagua hana uwezo wa kuchunguza utendakazi wa serikali.
Wajakoya ambaye ndiye kiongozi wa chama cha Roots Party ambacho alikitumia kuwania urais kwa uchaguzi mkuu uliopita. Hata hivyo Wajakoya alishindwa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kumaliza wa tatu na kushindwa na rais wa sasa William Ruto na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga mtawalia.
Kwenye mazungumzo amesema kuwa mienendo ya Gachagua akiwa ofisini haimuruhusu kuchunguza serikali.
Wajackoyah amemkashifu Gachagua na kumulaumu pakubwa kama aliyeongoza vita dhidi yao walipokua wakiongoza maandamano kutetea haki za wakenya.
Kiongozi huyo wa chama cha Roots Party amemtaka Gachagua kujitokeza waziwazi na kuomba msamaha kwa taifa bali si kujipendekeza kwa wananchi baada ya kubanduliwa mamlakani.
"wakati tulikuwa tunapigwa wakati wa maandamano, mtu kama Gachagua alikua anapiga sisi, kitu anafaa kufanya, atoke aombe msamaha kwa wakenya wote," Wajakoya alisema.
Wajackoyah pia ameonekana kujitenga na jambo la kuungana na Gachagua katika uchanguzi ujao.
"watu wanajitokeza wanasema tumeungana, mtu kama mimi siwezi ungana na Gachagua,"
Mwanasiasa huyo mwenye kisomo cha juu zaidi ametangaza hadhari kwamba atajitosa kwenye mbio za kuwania urais katika uchaguzi ujao 2027.
kiongozi huyo pia kwa upande mwingine ameilaumu serikali kwa kutotiza ahadi zake kwa wananchi namwananchi wa kawaida amelemewa na mzigo.
wajakoya ametaja kwamba ndio inayoweza kukidhi matakwa ya wananchi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!