MWANAMUME mmoja mwenye umri wa makamo amewastaajabisha watu mitandaoni baada ya kujiweka sokoni akitangaza kujiuza baada ya kuachwa na mkewe.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kupitia video yake kwenye mitandao wa video fupi wa TikTok, jamaa huyo alijirekodi akijipigia debe tayari kupata mnunuzi mpya – mwanamke wa kumchukua kama mpenzi wake.


Mwanamume huyo alielezea kwamba aliachwa na kulishwa block na mkewe kutokana na tabia yake ‘mbaya’ lakini akisema kwamba sasa ameshajirekebisha na yeye sasa ni mtu aliyebadilika.


Alisema kwamba mtu yeyote – haswa mwanamke, ambaye angependa kumchukua kama mpenzi wake, sharti alipe kiasi cha dola 17, sawa na shilingi 2,200 za Kenya.


Baadae, alirekebisha chapisho hilo akisema kwamba kulikuwa na makosa katika takwimu ya kwanza na kusema kuwa bei sasa ilikuwa ni dola milioni moja.


Chapisho hilo pia lina masahihisho ya ucheshi: "Haiwezi kuniondoa ??? Chapa na bei, kwa kweli ni $1,000,000 ?.”


Hata hivyo, chapisho hilo liliwazuzua watu ambao walifurika kwa maoni ainati. Haya hapa ni baadhi ya maoni;


aprilmcherron: "Mbona kama hii dili ni mbovu, mtu aliyebadilika kwa dola 17 ????."


 


Natalia?: "Ahh basi mtu ataniambia nitulie kidogo???siwahi kufanya vile??."


 


Lady_Benitas?: "Naapa nimeona yote kwenye App hii ??."


 


browniegoddess_: "Sitatulii hadi mwanaume anipende sana ????????."


 


kiaralavon: “hiki ndicho kitu kibunifu zaidi nilichoona hapa!!! Hawawezi kuondoa programu hii ????