Wanandoa maarufu wa Kenya Peter Kabi na Millicent Wambui wa The Wajesus family ni wazazi wenye furaha baada ya kumkaribisha mtoto wao wa tatu pamoja duniani.
Watayarishaji
wa maudhui hao wawili walitangaza kuzaliwa kwa binti yao Luxe Wajesus siku ya
Jumatatu katika chapisho zuri la video.
Wakati wa kutangaza habari hizo njema, wanandoa hao walimtambua binti yao kuwa mkamilifu na kufichua kuwa anafanana na Milly.
"Tusaidieni kumkaribisha Baby Luxe ulimwenguni! Yeye ni mkamilifu. Yaani anafanana tu na mamake!” Milly alisema kupitia Instagram.
"Hatuwezi kamwe kuchukulia kawaida baraka za kubeba mimba na kuzaa, ni muujiza wa kweli," aliongeza.
Mama huyo wa watoto watatu aliendelea kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa naye wakati wa safari yake ya ujauzito huku akitangaza mwanzo wa safari yake ya kulea.
“Sasa kazi ni kunyonyesha na kulea. Asante sana kwa jumbe zenu za pongezi,” alisema.
Hata kama wapenzi hao hawakufichua tarehe kamili ambapo mtoto wao wa tatu alizaliwa, ushahidi unaopatikana mtandaoni unaonyesha kwamba walimkaribisha mtoto wao siku kadhaa zilizopita.
Milly na Kabi Wajesus walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa tatu mnamo mwezi Septemba mwaka jana.
Wanandoa hao walitangaza tangazo hilo kwa mtindo kupitia video iliyoshirikiwa kwenye chaneli yao ya YouTube.
Video
ya tangazo la ujauzito ilichukuliwa jijini Dubai ambapo Milly alionekana akiwa
amesimama karibu na sanamu maarufu katika jiji hilo kabla ya kugeuka na kunasa ujauzito
wake.
Kabla ya tangazo hilo, wanandoa hao walikuwa wamewapa kazi mashabiki wao kukisia walichokuwa wakitaka kuuambia ulimwengu.
"Hii ni habari kubwa kwetu kwa mwaka wa 2024... hii ni ndoto kwangu," walisema.
"Ndio jamani tunakua na tunafuraha sana kuwa tumeshiriki nanyi habari hizi njema,"
"Sisi kila wakati tunasema kuwa wakati mzuri ni bora kwa kupata mtoto kwa ajili ya kutangaza, kwa kuruhusu ulimwengu.
"Tuna furaha kwa kubarikiwa na mzaliwa wetu wa tatu - mtoto wetu wa tatu," wenzi hao walisema kabla ya Kabi kuombea ujauzito huo.
Wanandoa hao pia walikiri kwamba wanafurahi kufanya ufunuo wa ujauzito huko Dubai.
"Mimi ndiye mwanamke mjamzito mwenye furaha zaidi kuwahi kutokea, na tafadhali tupe jina la mtoto," Milly alisema.
"Naweza kupata watoto 10 na wewe kwa sababu unafanya uzazi wa ajabu sana," Kabi alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!