MCHUNGAJI wa kanisa la Neno Evangelism, James Maina Ng’ang’a kwa mara ya kwanza ameunga mkono juhudi za serikali kuwaadhibu vijana wanaotumia teknolojia ya akili mnemba kuweka viongozi kwenye majeneza.
Katika mahubiri yake wiki jana, Ng’ang’a alisema kwamba yeye pia haungi mkono tabia hizo za kutumia AI kumweka mtu aliye hai kwenye jeneza kana kwamba ni maiti.
Alisema kwamba pia yeye amekuwa mwathirika wa hulka hiyo ambapo amekuwa akiona picha yake imewekewa pombe mbele yake, na kulaani vitendo hivyo.
“Sina furaha, nakumbuka yule kijana alikuwa ananiweka sufuria kwa kichwa, nilitoa onyo awali. Vitu vingine ni vya kiroho, tunaweza omba na kuwasaidia wale vijana. Vitu vingine si poa, mimi siungi mkono mtu kuchukua mfalme na kumweka kwenye jeneza,” Ng’ang’a alisema.
“Siungi mkono kabisa mtu kuchukua picha yangu anakata hapa na kuniwekea chupa ya pombe hapo…wakati mwingine nyinyi vijana mjue kwamba licha ya hayo yote, mnafaa kufikiria mara mbili. Huwezi kuniharibia mimi jina hivi, jina ambalo nimetengeneza kwa muda krefu tangu kutoka gerezani,” alifoka.
Mchungaji huyo alisema kwamba anamuunga mkono waziri wa masuala ya usalama wa ndani Kipchumba Murkomen kwamba watawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria mtu yeyote anayewaweka viongozi kwenye majeneza.
‘Ahsante sana waziri, shika hao watu. Mwenye kupost hivyo vitu mkamate, CS niliona umesema, hiyo ni hatua nzuri. Hapo nakuunga mkono, washike hao watu na waweke Kamiti, na wasipewe dhamana.’
“Nasema siungi mkono mtu kuchafulia mwingine jina, kuweka mtu kwa jeneza, kuwekea mtu pombe, unachukua msichana unaniwekea hapa na ni kompyuta mnatumia, hiyo ningeomba tu watu washikwe na wasipewe bondi kwa sababu wengine hawajui,” Ng’ang’a aliongeza.
Aliwataka waombezi kujumuika kwa ajili ya kuomba na kuombea nchi kwa vile hulka kama hiyo imekuwa ikikithiri sana.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!