SARAH Mtalii, MD wa kampuni ya utalii ya Bonfire Adventures amefichua kwamba aliondoka katika ndoa yake na mapema mwaka 2022.
Akizungumza na Dr Ofweneke kwenye podikasti yake ya Lessons @30, Sarah alifichua kwamba hisia zake zilihama kabisa kutoka kwa ndoa na Kabu mapema 2022 japo amekuja kuondoka kabisa kimwili mwishoni mwa 2024.
Alisema kwamba kauli hiyo si geni kwani ni kawaida kwa wanawake wengi kuondoka katika kitu kihisia mwanzo kabla ya kuondoka kimwili baadae.
Alikiri kwamba kati ya 2022 na 2024, amekuwa akining’inia tu katika ndoa yake na Simon Kabu japo kihisia, aliondoka hiyo 2022 mapema.
“Niko katika amani, na nafikirio unaweza niambia, ninaonekana kama mtu ako na mawazo? Unajua kwetu sisi wanawake, nimekuja kugundua kwamba tunaondoka kwa ndoa kama miaka miwili mitatu kabla ya kuja kutoka sasa kimwili,” Sarah alisema.
“Wanawake huwa tunaanza kuondoka kiakili, kihisia na mwishoni tunatoka kimwili. Mimi niliondoka kitambo lakini bado nilikuwa pale. Sijui nasikia watu wakisema nilikuwa tu nimening’inia ndani pale.”
‘Kihisia nafikiri naweza kusema niliondoka mapema 2022,’ Sarah aliongeza.
Mjasiriamali huyo alifichua kwamba kitu ambacho kilikuwa kimemfanya kuning’inia kwa muda huo wote wa zaidi ya miaka miwili ni watoto lakini pia biashara yao ya Bonfire Adventures.
“Mwanzo ninaweza sema kwamba watoto walinifanya nikabaki pale kwa muda. Unajua mimi nimelelewa maisha ya kikamilifu na tamanio langu lilikuwa kuona wanangu wakikulia maisha kama hayo ambapo kuna mama na baba kwa sababu ninaamini kwamba kila mzazi ana nafasi yake katika makuzi ya mtoto…”
“…kuna nafasi ya baba ambayo nilikuwa najua hata nikienda kule nje sitaweza kuijaza, lakini nimekuja kugundua kwamba ni jambo linawezekana tu,” alifunguka.
Sarah alisema kwamba kwa sababu biashara yao ilikuwa katika kasi nzuri, walikuwa wanalazimika kusafiri kujivinjari ambapo wangelala katika vyumba tofauti.
“Wakati mwingine ningelazimishwa hata kuenda kwa ‘holidays’ ambapo tungelala kwa vyumba tofauti au vyumba pacha,” Sarah alisema akisistiza kwamba hilo lingefanyika kwa ajili tu ya kibiashara.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!