MCHUNGAJI wa kanisa la Neno Evangelism Centre, James Maina Ng’ang’a amewarai wanawake na haswa wale walioko katika ndoa kukoma kutumia mitandao wa Facebook.
Akizungumza katika mahubiri yake siku mbili zilizopita, mchungaji huyo alidai kwamba mitandao ya kijamii na haswa mitandao wa Facebook unatumika kama mawindo na shetani.
Mchungaji huyo alisema kwamba watu wengi wanaoabudu shetani wamejaa katika mitandao wa Facebok wakitafuta watu wa kuajiri katika Imani yao, lengo kuu likiwa wanawake wa watu.
“Mnajua jinsi wanaunganisha watu kwenye ‘devil worshipping’? Kuna devil worshipper, kuna iluminati, kuna wachawi na kuna wazimu. Unajua siku hizi wanafanya nini? Wanakuja kwa Facebook, na ndio naambia kina mama wale ambao hamna kitu mnafanya tokeni Facebook,” James Ng’ang’a alisema.
“Hapo Facebook kuna uchawi ambao hamtaweza. Wake wa watuv tokeni Facebook, hapo kuna vitu ambavyo hamtaweza. Msifanye mchezo na Facebook, unaenda kote duniani. Na kuna watu hapo wanafungua link na anakutumia ujumbe, ukifungua huo ujumbe tu, nyingine huwa zimeandikwa ‘hi’. Ukishajibu tu kuna vitu wanafanya unajikuta tayari umeshaingia kwao,” alichambua.
Ng’ang’a alieleza kwamba baadhi ya watu hao hutumia wanawake warembo ambao hujifanya kuwa wanatafuta wanaume wa kuwa marafiki zao.
Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa hekaya kama hizo kuenezwa kwamba mitandao ya kijamii inatumika kuwachukua watu katika itikadi zisizostahili.
Ni dhana ambazo imekuwepo kwa muda japo hatuwezi kubaini ukweli wake.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!