MCHUNGAJI wa kanisa la Neno Evangelism, Apostle James Maina Ng’ang’a amedai kwamba utabiri wake kuhusu ujio wa mapepo nchini Kenya umetimia.
Katika mahubiri yake siku chache zilizopita, Mchungaji Ng’ang’a alisema kwamba siku kadhaa zilizopita, alitoa utabiri kuhusu mapepo mabaya kuvamia Kenya kutoka mataifa ya ughaibuni.
Mchungaji huyo hata hivyo alisema kwamba kuna baadhi ya wateule ambao wameitwa na Mungu na ambao watasimama tisti dhidi ya mapepo hayo, akitoa rai kwao kufanya kazi hiyo kwa uadilifu.
“Sasa wachache wale ambao mnanisikiliza, kuna wale Mungu atawaita msimame mpigane na mapepo yale makubwa yanayokuja Kenya. Niliambia Wakenya miaka iliyopita kwamba nilikuwa na maono shetani akitafuta mahali pa kutua hapa Afrika na ni nchi ya Kenya,” Ng’ang’a alisema.
“Nakumbuka nikiambia watu wafunge milango, basi sasa shetani ashaingia, yuko hapa. Kenya ni miongoni mwa mataifa ya kishetani. Iko katika taratibu zile za mapepo,” Pasta Ng’ang’a aliongeza.
Mchungaji huyo aliendelea kueleza kwamba mapepo ni vitu ambavyo vinaishi kiroho huku akieleza jinsi mtu anaweza kubaini kama ana mapepo.
“Mapepo ni vitu ambavyo vinaishi kiroho, hayaishi kimwili. Lakini utaweza kuona matendo yake. Ukitaka kujua uko na pepo wewe, ukipata pesa zako zimepangwa na shetani vile zitaenda.”
“[Ukisikia mtu akisema] najua hamtanichagua 2027, wewe uko na pepo!” aliongeza.
Mchungaji huyo pia alisema kwamba mwanamke yeyote anachumbiwa zaidi ya mara mbili bila kuolewa, hiyo ni ishara Dhahiri ya kukaliwa na mapepo.
“Umekatiwa na wa kwanza, wa tatu hadi wa nne… watu 50 hadi 200 wanakukatia na hawakuoi sababu uko na mapepo ya ‘delay’. Pepo hili lengo lake ni likukule urembo wako mpaka uishe. Na kama si hivyo, wakupatie mtu ‘wrong number’. Sasa hivi shetani anapeana ndoa, unapata mtu ndoa inakaa miaka 3 inavunjika,” Ng’ang’a alihubiri.
Ng’ang’a alijitolea mfano akisema kwamba mtu asiye na mapepo huwa hachelewi kuoa au kuolewa. Alisema kuwa yeye aliokoka 1992 na mwaka uliofuata akafanya harusi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!