KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Januari 16.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Bomet, Nandi, Nyeri , Kiambu, Kilifi.

Katika kaunti ya Bomet, sehemu za eneo ya Mulot na mji wa Bomet zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Kaptumek katika kaunti ya Nandi litaathirika kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Maeneo ya Kimathi University na Hill Farm katika kaunti ya Nyeri yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu za maeneo ya mji wa Ruiru, Mugutha, Tigoni Tea, Limuru Girls, Gitiha, na Kiawaroga zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Kokotoni katika kaunti ya Kilifi pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.