SARAH Mtalii, afisa mkuu wa kampuni ya Bonfire Adventures amefichua kwamba kabla ya kutulia katika ndoa, aliwahi chumbiana na wanaume wenye taaluma nzuri tu.
Akizungumza na Dr Ofweneke, Sarah alisema kwamba katika umri wake wa kati ya miaka 20-30, alichumbiana na wanaume wenye taaluma nzuri lakini wote hawakumvutia kuolewa na hata mmoja wao.
“Katika umri wangu wa 20-30, nilikuwa nimekutana na watu lakini sikuwahi vutiwa na mmoja wao. Nilikuwa sasa natafuta mwanamume wa kunioa,” alisema.
“Nilikuwa natafuta mwanamume lakini sidhani walikuwa tayari kuwa wanaume. Sitaki kuwahukumu lakini walikuwa ni watu wazuri. Pia mimi nilikuwa na chaguo langu katika mwanamume. Nilikuwa natafuta mwanamume wa nguvu. Nafikiri nilichumbiana na rubani, mtaalamu wa IT, mhandishi wa ujenzi wa nyumba… ni vile sitaki kuwataja tu maana watu wanaweza wajua,” Sarah Kabu alisema.
Alieleza kwamba hata aliwahi chumbiana na mwanaume mwenye utajiri wa kiwango cha bilionea lakini bado hakuvutiwa katika ndoa na yeye.
Mama huyo alieleza kwamba licha ya kuchumbiana na watu wa kipekee, aligundua kwamba watu wenye majina makubwa ingemkalia vigumu kukaa nao na hapo ndipo aliamua kwamba roho yake inataka mtu wa kawaida tu.
“Nilichumbiana na watu wa ajabu lakini niligundua hawa watu wa majina makubwa itanikalia vigumu kuwa nao hivyo nikasema ninataka mtu wa kawaida. Nafikiri wakati mwingine wale watu wenye majina makubwa pengine huwa wanataka tu kujibamba lakini hawako tayari kuoa, na kwangu mimi nilikuwa natafuta mume. Na ndio maana ilinikalia rahisi kuwaacha wote, hata mmoja wao alikuwa bilionea,” Sarah alisema.
Sarah alifichua kwamba kabla hajaolewa, alikuwa anawaogopa sana wanaume watanashati, japo alikiri kwamba baadhi ya ma’Ex wake walikuwa watanashati wa ajabu.
‘Pengine naweza sema kwamba kwa wakati huo kwa kweli nilikuwa nawaogopa sana wanaume watanashati japo baadhi ya maEx wangu walikuwa watanashati kupindukia. Nilikuwa nawaogopa sana kwa sababu unajua kila mwanamke anawataka,’ Sarah alifichua.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!