MSANII wa Marekani, Chris Brown ameguswa na video zinazosambaa kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikionyesha hali ya kutamasha ya vijana waliohukumiwa kunyonywa.
Awali tuliripoti kwamba zaidi ya vijana 170 wanaoaminika kuwa wanachama wa kundi la Kuluna Gang linalwahangaisha watu mijini walipatikana na hatia na kuukumiwa kifo kwa kunyongwa.
Video ambazo zimekuwa zikisambaa zinaonesha vijana hao wakiwa katika hali ya majonzi wakati walikuwa wanasafirishwa kwenda kunyongwa.
Chris Brown alichukua kupitia Instagram yake na kusema kwamba video hiyo inakata maini sana na inaashiria jinsi utu na ubinadamu umeyeyuka miongoni mwa watu.
“Nyinyi wote mumeona video zile zinazotoka nchini Congo? Kitendo kile kinavunja moyo sana na kinakosa utu,” Chris Brown alisema.
Kwa mujibu wa mashirika ya Habari ya kifamaita, Sabini kati ya wafungwa hao walisafirishwa siku ya Jumapili wiki jana, Waziri wa Sheria wa Kongo Constant Mutamba alisema, akiongeza wafungwa wengine 102 ambao tayari wamepelekwa katika gereza la Angenga katika jimbo la kaskazini la Mongala.
Vijana hao wa kati ya miaka 18-35 wamepatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha na wanajulikana kama "Kulunas" au "majambazi wa mijini."
Wana umri wa kati ya miaka 18 na 35, Mutamba alisema katika taarifa. Hakusema ni lini mauaji yatafanyika
Japo taarifa zingine zinasema vijana hao bado hawajanyongwa, vyanzo vingine vinadai kwamba angalau 100 kati yao wameshauliwa.
Kongo ilifuta hukumu ya kifo mwaka 1981, lakini ilirejeshwa mwaka wa 2006. Unyongaji wa mwisho ulifanyika mwaka wa 2003.
Mnamo Machi 2024, serikali ya Kongo ilitangaza kuanza tena kwa adhabu ya kifo katika kesi za uhaini zilizofanywa na wanajeshi.
Mnamo Mei, wanajeshi wanane walihukumiwa kifo, na mnamo Julai, wanajeshi 25 walitiwa hatiani kwa makosa kama hayo. Hakuna anayejulikana kunyongwa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!