BAADA ya miezi kadhaa ya kuwapa furaha watumizi wa Android, program ya Songa Play sasa imetanua mbawa za huduma zake za burudani hadi kwenye iOS, kama njia moja ya kuwajali watumizi wa vifaa vya Apple pia.
Songa Play, ambalo ni jukwaa la kipekee linalokupa burudani ya vipindi vyote vya Radio Jambo na muziki kwa saa 24 kila siku, sasa linaweza pakuliwa si tu kupitia PlayStore lakini pia kwenye IOS.
Hili ni jukwaa la kidijitali lililobuniwa na shirika la Habari la Radio Afrika ili kuwajali mashabiki wa vipindi vyote vya Radio Jambo.
Uzuri wa kuwa na Songa Play kwenye simu yako, unaweza kufuatilia vipindi pendwa kama vile Patanisho ya Gidi na Ghost, DeadBeat ya Massawe Japanni, Toboa Siri na Mbusii na Lion miongoni mwa vipindi vingine, popote na muda wowote.
Jukwaa hilo lilizinduliwa takribani miezi 5 iliyopita kwa watumizi wa vifaa vya Android, lakini sasa linafurahia kutaarifu umma kwamba hata wale wanaotumia vifaa vya Apple wanaweza kufurahia vipindi vya Radio Jambo na muziki kwa kupakua program hiyo ambayo sasa inapatikana kwenye IOS.
Stesheni zote, zikiwemo Radio Jambo, Kiss 100 FM, Classic 105, Gukena FM, Home Boyz na East FM zina vipindi vyao vyote katika jukwaa la Songa Play ambavyo vinapeperushwa kwa saa 24 kila siku.
Vipindi hivyo ni pamoja na podkasti pendwa zinazoifanya stesheni ya Radio Jambo kupepea na kutawala mawimbi ya utangazaji Kenya kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Kama una simu yako ya mkononi, iwe Android au iPhone, sasa unaweza ukajumuika na mamilioni ya watu wanaopata burudani lisilo na kikomo kwa kujisajili bila malipo kwenye Songa Play kupitia www.songaplay.com au kupakua program kupitia Play Store au IOS.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!