Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi alimjibu vikali waziri wa utumishi wa umma Justine Mturi
kuhusiana na madai aliyotoa Januari 13 kuhusu utekaji nyara unaoendelea,
akirejelea kutekwa nyara kwa mwanawe Leslie Muturi mwezi Juni mwaka jana wakati
wa maandamamano ya Gen-Z .
“Hii njia ya Muturi ni ya kuudhi. Hili linakuja wakati ambapo nafasi yake katika siasa ameonesha kujaribu kusalti hasa wakati huu ambao kuna mtafaruku katika taifa. Huku kunaonesha tu anatafuta umaarufu katika siasa. Kuhusiana na maswala na makosa ya mwanawe ambaye ni rika yangu. Kwani mwanawe alishikwa pasipo sababu.”
Sudi pia aliongeza kwamba matamshi ya Muturi ni kusaliti serikali ya kenya kwanza. Alimtaka Muturi kujiuzulu badala ya kuendelea kuichimba serikali ambayo yuko ndani yake.
“Kuna watu wengi ambao wanaezafanya kwa serkali kazi nzuri tena kiungwana katika kaunti ya Embu, ukichoka jiuzulu,” aliongeza Oscar Sudi.
Kwenye barua aliyoandika jana Januari 14 katika kituo cha polisi alivyotakiwa kufanya na vyombo vya usalama, Muturi alieleza kwamba kuna haja ya serikali kuchukulia manani swala la utekaji nyara, huku akifafanua kwa kina kilichofanyika wakati mwanawe alikuwa ametekwa nyara na waliodaiwa kuwa maafisa wa usalama
Waziri Muturi alieleza madai yake yote ya utekaji nyara kwa mwanawe na alivyojaribu kutafuta usaidizi kwa viongizi wakuu serikalini pasipo mafanikio.
Hili lilimfanya kuenda ikulu kumtafuta rais baada ya ujumbe alioutuma kwa rais kufeli kufika.
Rais Ruto
alipomtafuta mkuu wa DCI Noordin Haji ndipo Haji alikiri kuwa mwanawe
Muturi Leslie muturi yuko na ataachilia
chini ya lisaa limoja.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!