KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Januari 15.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Bomet, Nyeri, Kiambu, Nandi, Turkana, Kitui, na Kilifi.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Dandora, na Westlands zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za eneo la Mulot Feeder katika kaunti ya Bomet zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kiawara, Nairutia, Gatunganga, na Ngorano katika kaunti ya Nyeri pia zitaathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ya Juja Farm, Athi Spur, Komo Spur, na Munyu Feeder yataathirika kati ya saa tatu asuubuhi na saa sita adhuhuri.
Eneo la Maraba katika kaunti ya Nandi litaathirika kati ya saa mbili na robo asubuhi na saa kumi na moja unusu jioni.
Sehemu za maeneo ua Katilu na Kalemngorok katika kaunti ya Turkana zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Mulutu, Katulani, Kavisuni na Kanyangii katika kaunti ya Kitui pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa sita adhuhuri.
Sehemu za maeneo ya Kanamai na Kikambala katika kaunti ya Kilifi yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!