MSANII na mkuza maudhui kupitia YouTube, Diana Marua amefunguka jinsi alipambana na maisha ya kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii mwanzoni mwa ndoa yake na msanii Bahati Kioko.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana Marua alipakia picha ya kumbukumbu kutoka miaka 7 iliyopita alipokuwa na mimba ya mwanawe wa kwanza, Heaven Bahati.
Alisema kwamba mimba hiyo ilikuja na hisia mseto, kwa upande mmoja akiwa na furaha ya kutarajia kuitwa mama huku kwa upande wa pili akiwa maskini bila kazi wala pesa.
“Snapchat ilinikumbusha siku kama hii, miaka 7 iliyopita ??♀️ Nilikuwa na takriban 90kgs hapa, na kujenga kumbukumbu ya picha ya mtoto wangu mapema. Mwezi mmoja baadaye, nilimshika Mtoto wangu, mrembo kuliko wote, Heaven - mikononi mwangu,” Diana alisema.
Mama huyo wa watoto watatu wa kuwazaa alifichua kwamba mimba yake ya kwanza ilimpitisha katika nyakati ngumu, kiasi kwamba watu walianza kunong’ona mitandaoni kwamba Bahati alioa mwanamke mkubwa kumliko.
“Mimba ilininyenyekeza. Hakuna kazi, hakuna ndoto, hakuna mwelekeo. Walisema, Bahati alioa kwa ‘Shosh’ ??? Njoo ufikirie hilo, nyote mlienda mbali kidogo ? Wachambaji wa mitandaoni,” Diana aliwasuta waliosema hivyo.
Diana alisema kwamba haikupita muda mrefu kabla ya Mungu kufungua njia zake za mafanikio na anapoangalia nyumba, anabaki tu kurudisha shukrani kwa Mungu.
‘Mungu alikuwa na mpango. Ilikuwa ni suala la muda tu. Nilikuwa na mtu sahihi kando yangu, mshangiliaji wangu mkuu. Nilikubali mabadiliko, sikujali kidogo, niliamini safari yangu, na Mungu alipanga maisha yangu,’ alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!