
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Januari 14.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Bomet, Kiambu, Nandi, Nyeri, Kilifi na Mombasa.
Katika kaunti ya Bomet, sehemu za Siongiroi Feeder zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za Tola, Bob Harris, Ngoingwa, Metro, TIBS, Compuera, Evergreen, na Gitamayu katika kaunti ya Kiambu zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Maraba na Kibwareng katika kaunti ya Nandi pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Major Seminary na Njeng'u yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za mji wa Kilifi katika kaunti ya Kilifi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Wakati huo huo, sehemu za maeneo ya Bombolulu na Bamburi katika kaunti ya Mombasa pia yataathirika.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!