MSANII na mjasiriamali kutoka Tanzania, Diamond Platnumz amewatayarisha kisaikolojia mashabiki wake kuhusu ujio wa albamu yake mpya.
Kupitia kwa Instagram yake siku chache zilizopita, msanii ambaye anamiliki chombo cha Habari cha Wasafi na lebo ya WCB Wasafi alifichua kwamba ataangusha magoma ya kipekee katika albamu yake ijayo.
Diamond alithibitisha kwamba albamu hiyo itatoka kabla ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan, akiipaisha kuwa yenye itawakumbusha mashabiki wake kwa nini yeye ni ‘simba’.
Msanii huyo alisema kwamba licha ya wengi kuona ngoma zake za miaka miwili iliyopita – Zuwena na Yatapita kama ngoma bora kutoka kwake, ngoma mpya zilizopo katika albamu hiyo zitawafanya kuona hizo nyimbo mbili kama uchafu tu.
“Albamu mpya ya Bongo Fleva kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Achana na Zuwena, Yatapita, hizo ni uchafu,” Diamond aliandika.
“Nataka niwakumbushe nini kilifanya nikapendwa,” Platnumz aliongeza huku akisisitiza kwamba albamu hiyo itakuwa na upekee wa ngoma za Bongo Fleva pekee bila mchanganyiko wa mtindo mwingine wa muziki.
Msanii huyo licha ya kufanya vizuri katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa mkimya sana likija ni suala la kuachia albamu, kwani mara ya mwisho alitoa albamu ilikuwa mwaka 2022 alipoachia EP ya FOA.
Tangu alipoachia ngoma hizo mbili ambazo sasaameita uchafu, Diamond ameonekana kutoka nje ya mdundo wa Bongo Fleva na nyingi ya ngoma ambazo ameachia ni za mdundo wa Amapiano.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!