TIKTOKER Rachel Otuoma amewashukuru wanajamii ya TikTok kwa kusimama naye katika takribani kipindi cha miaka 5 ya ugonjwa wa marehemu mumewe, mwanasoka Ezekiel Otuoma.
Mrembo huyo alizungumza kwa ujasiri wakati wa mazishi ya mumewe Jumamosi Janauri 11 katika kaunti ya Siaya na kuwashukuru TikTokers kwa kusimama naye kuhakikisha Otuoma hakuwahi kosa dawa wala chakula katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
“Ningependa kushukuru kila mtu, na haswa familia yangu ya TikTok, wueh! Nyinyi watu mmenishikilia kama Otuoma yuko, mmenishikilia kama sasa hivi vile hayuko… tiktokers, ahsante za dhati kwenu,” Rachael alishukuru.
“Ningekosa hata dawa, nilikuwa naenda hapo kwa hiyo TikTok, nitachambwa lakini kuna mmoja atajiotokeza anunue dawa. Hivyo TikTok ni familia yangu. Sikuwahi kosa hata chakula, kama niko hapo TikTok. Otuoma alikuwa anwafinyia jicho, anawatabasamia na mlikuwa mnafurahia, hivyo kwangu TikTok ni familia kubwa sana,” alisema.
Rachael alisema kwamba mwaka huu ndio wangetiiza miaka 10 ya ndoa na Ezekiel Otuoma, huku akimtaja kama mwanamume aliyempa heshima ambayo wanawake wengi hawapati maishani.
“Mkiangalia, hapa si kwamba ninamzika mume wangu kumsahau, hii ni kama kumbukumbu ya 10 ya ndoa yetu. Huu mwaka tungeadhimisha miaka 10. Mkiniangalia hivi mimi ni mwanamke mkakamavu sana. Hakuna kitu kingine kinaweza nitingisha juu ya huyu mwanamume.”
“Nitaendelea kumpenda huyu mwanamume hata kama ako hapa chini, huyu mwanamume alinipa heshima yenye wanawake wengine hata hampati hapo nje. Na bado nitampa hiyo heshima hata kama hayuko nando yangu,” Rachel aliomboleza Ezekiel Otuoma.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!