MUIGIZAJI Sandra Dacha amefichua kwamba safari yake ya kupunguza uzani wa mwili wake imekuwa ikizaa matunda chanya kwa miezi minne sasa.
Mrembo huyo mwenye unene alisema kwamba aliamua kuingia katika safari ya kupunguza uzai baada ya kushauriwa na daktari kwamba alikuwa amefika hatua ya mwisho kabisa katika unene, ambayo si ishara nzuri kwa afya yake.
Hapo ndipo aliamua kutafuta njia ya kupunguza uzani wake, na ana furaha kwamba miezi minne baadae, amepunguza angalau hai kilo 17 na anafurahia maendeleo ya safari yake ya kukata uzito.
“Nilihisi mgonjwa, nikaenda hospitalini, nikapimwa na nikagundulika kuwa nina nimonia. Nesi alinivuta pembeni akaniambia ni muhimu ikiwa nitapunguza uzito kwa sababu nilikuwa nimezidi unene?i was now at "GREATER MORBID OBESITY" Hizi ni hatua za mwisho za unono?hapa ukipita sasa wewe tunakuwachia tu Mungu.”
“Ili kufupisha hadithi ndefu...niliamua kutafuta suluhu na ndipo nilipokutana na @dr_arshni_malde wa @tiaclinicskenya na Kuanza safari yangu ya kupunguza uzito OZEMPIC Agosti mwaka jana…huu ni mwezi wangu wa Nne na ninaupenda? Nilikuwa na uzito wa kilo 152 na leo nina 135kgs. Kupunguza kilo 1 kwa wiki,” Dacha alisema.
Licha ya ‘The Biggest Machine’ kufurahia kupunguza uzani kutoka kilo 152 hadi 135, bado anahisi safari yake ingali mbali kutoka kufika mwisho kwani analenga kupunguza hai angalau 115kgs.
Alisema kwamba awali kabla aache kuzingatia ongezeko la unene wa mwili wake, alikuwa anatembelea uzani wa kati ya kilo 115 na 123.
Dacha alisema kwamba alikuwa anataka kuweka kama siri safari yake ya kupnguza uzani lakini aligundua baadhi ya watu wameshaanza kushuku kutokana na picha zake mtandaoni za hivi karibuni.
“Nina safari ndefu. Uvumilivu ni muhimu. Ninataka kurejea kilo zangu za kawaida…115,123 hapo. Nilitaka kushiriki safari yangu ya kupunguza uzito baada ya mwaka mmoja lakini nimekuwa nikisoma sehemu ya maoni wakati wowote ninapochapisha na ni wazi nyie walikuwa wameanza kuniona nikipungua uzito hivyo nikasema kwanini nisiongee kuhusu hilo sasa??♀️ ama niko na kiherehere,” alimaliza kwa utani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!