BINTI wa rais, Charlene Ruto ametangaza ujio wa shindano lake jipya kwa vijana ambalo litafanyika mwezi ujao.
Kupitia ukurasa wake wa X, binti wa kwanza wa rais Ruto alifichua kwamba vijana wenye talanta katika ubunifu wa mitandaoni wenye kati ya umri wa miaka 18 hadi 35 wanaweza jiandikisha.
Alisema kwamba ili kujisajili, vijana ni sharti wajiunge kwa makundi ya watu 3 na kuonyesha ueledi wao katika suala la kubuni wavuni, kujisajili kutaendelea hadi Februari 11.
“Ni wakati wa jambo letu kubwa linalofuata…. Mashindano ya Tovuti! Je, wewe ni kati ya miaka 18-35? Ungana katika vikundi vya watu 3 na utuonyeshe ulichonacho! Changamoto itafunguliwa: 11 Januari 2025. Makataa ya kuwasilisha: 11 Februari 2025, saa sita usiku. Hatua za kuhitimu:
1 Shiriki viungo vya tovuti 3 bora ambazo timu yako au wanachama wameunda.
2️⃣ Tutumie pendekezo fupi la kiufundi la tovuti ambayo ungeunda kwa ajili ya TYPNI.
3️⃣ Ambatisha vitambulisho na wasifu wa washiriki wote 3 wa timu.
Shinda $1,500 USD! Wacha tuone ubunifu wako unang'aa. Tayari? Hebu tufanye hivi!” Charlene aliandika.
Hii si mara ya kwanza kwa binti wa rais kutangaza shindano la kuwakimu vijana wenye ujuzi katika ubunifu wa mtandaoni.
Mwaka jana, binti Ruto alitangaza shindano sawia na hilo lililofanyika majira sawia, na tuzo kwa mshindi ilikuwa shilingi laki moja taslimu.
Kando na taslimu, Charlene Ruto wakati huo alitangaza kula chakula cha mchana na mshindi katika mgahawa wa kifahari.
“Mtandao wa Vijana wa Kimataifa (TYPNI) unatafuta nembo bainifu inayojumuisha ari ya ujana na ubunifu. Shindano hili linatoa fursa kwa wabunifu wachanga kuonyesha vipaji vyao na kuchangia utambulisho mahiri wa TYPNI,” aliandika kwenye bango hilo kwenye mtandao wa X.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!