MSHAWISHI maarufu kupitia mtandao wa X, Eric Amerix ni miongoni mwa wazazi ambao wanasherehekea wanao kupita vizuri katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne, KCSE.
Kupitia ukurasa wake wa X, Amerix alijiunga na maelfu ya wazazi wengine kusherehekea wanawe 3 ambao walikuwa miongoni mwa watahiniwa zaidi ya laki 9 waliokalia mtihani huo mwishoni mwa mwaka jana.
Mshawishi huyo alihadithia jinsi wanawe watatu, wote wavulana walivyopasi katika mtihani huo matokeo yake yaliyotangazwa Alhamisi na waziri wa elimu Julius Migos Ogamba.
Alifichua kwamba mmoja wa wanawe ambaye mwaka 2023 aliigiza kama ‘Zakayo’ – mtu wa kutoza ushuru, alipata B+ na kwamba ndoto yake ni kuwa afisa wa mamlaka ya kutoza ushuru.
“Eljay (mwenye rangi ya kijani, kulia kabisa) alipata B+ (Plus). Aliigiza kama mkaguzi wa serikali mnamo 2024. Mnamo 2023, aliigiza kama ZAKAYO, mtoza ushuru mkatili. Ndoto yake ni kuwa Mkurugenzi wa Mapato na Ukusanyaji wa Kodi,” Amerix alifichua.
Alisema kwamba wanawe wote watatu walifanikiwa kutoka shule ya upili ya Kamusinga na kueleza ndoto ya kila mmoja.
“John (mwenye kaptura nyeupe), ambaye aliibuka MWIGIZAJI BORA wa taifa mwaka wa 2023 na 2024, amepata B+ (Plus). Rushel (mfamasia, mwenye koti jeupe na vichaka vya buluu) alifunga A (Plain). Ndoto yake ni kuwa mfamasia. Ndio maana alitenda vyema katika nafasi hiyo,” alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!