KAMATI inayoongoza maandalizi ya safari ya mwisho ya mwanawe mtangazaji wa Radio Jambo, Lion Deh imetoa ratiba ya jinsi mazishi yatafavyofanyika.


Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Master Lion atazikwa Jumamosi ya Januari 11 katika boma la wazazi wake katika kaunti ya Kakamega.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Ibada ya kuombea wafu imefanyika leo Ijumaa ya Januari 10 katika makafani ya Montezuma huko Mbagathi, jijini Nairobi.


Baadae, mwili wa mtoto huyo utasafirishwa kwa ndege hadi Kisumu kabla ya kusafirishwa kwa barabara hadi nyumbani kwao katika kijiji cha Eshiongo, Eneobunge la Khwisero kaunti ya Kakamega.


“Tutakuwa na ibada ya wafu kwa ajili ya Lion Master kesho (Ijumaa) asubuhi saa 10 katika barabara ya Montezuma mbagathi, kisha tutasafiri kwa ndege hadi Kisumu kwa ajili ya safari ya mwisho ya kumuaga Lion katika kijiji cha Eshiongo, eneo bunge la khwisero, Kaunti ya Kakamega Jumamosi tarehe 11 Januari 2025,” taarifa ilisema.


Mwanawe Lion, mwenye umri wa mwaka mmoja alifariki siku chache zilizopita kufuatia majeraha makali aliyoyapata baada ya kuanguka.


Taarifa ya familia ilisema kwamba mtoto huyo aliathirika sehemu kubwa ya ubongo wake kumpelekea kulazwa hospitalini katika chumba cha wagonjwa mahututi.


Mtoto huyo alianfuka sakafuni kutoka kwa sofa sebuleni alikokuwa akicheza na wenzake.