MTANGAZAJI wa miziki ya Reggae kupitia stesheni ya Radio Jambo, Lion Deh amefunguka kwa undani mazingira ambayo mwanawe alipatana na umauti.
Katika sasisho jipya kutoka kwa familia, Lion Deh alikanusha uvumi unaoenezwa mitandaoni kwamba mwanawe alidondoka kutoka ghorofani.
Mtangazaji huyo alibainisha kwamba Mwanawe, Master Lion alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka kutoka juu ya sofa alikokuwa akicheza sebuleni.
Lion Deh aliwashukuru mashabiki na marafiki kwa jumbe za kumfariji ambazo zimetiririshwa kwake katika kipindi cha siku chache tangu taarifu hizo za kuvunja moyo zilipowekwa wazi kwa umma.
“Asante kwa jumbe zanu za kufariji na maombi wakati mimi na familia yangu tunapojaribu kukubali mapenzi ya Mungu. Master Lion alianguka kutoka kwenye sofa la sebuleni wakicheza ndani ya nyumba SIO KUTOKA kwa balcony,” sehemu ya sasisho hilo jipya ilisomeka.
Mtangazaji huyo alisimulia kwamba huo ndio ulikuwa mwanzo wa mahangaiko ya kutafuta matibabu kwa mwanawe ambaye madaktari walisema alipata jeraha baya kichwani na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa sehemu ya ubongo wake.
“Tulimkimbiza katika kituo cha matibabu cha karibu hospitali ya mji mkuu na baada ya uchunguzi wa CT scan iligundulika kuwa alikuwa na damu ndani ya kichwa hivyo alikimbizwa kwa upasuaji wa saa 3 ambao ulifanikiwa, lakini kutokana na hali ya jeraha ubongo ulikuwa umeteseka na kuanza kuvimba, aliwekwa ICU kwa madaktari wakitarajia uvimbe utakoma, lakini haikuwa hivyo kwani jeraha la ubongo lilikuwa kubwa huku matabibu wakieleza kuwa ubongo umekufa na hakuna kitu zaidi wangeweza kufanya,” taarifa hiyo ilisema.
Alifichua kwamba wakati huo wote, maisha ya mwanawe yalikuwa yakisaidiwa kwa mashine maalumu kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na hatimaye alifariki majira ya saa moja asubuhi ya Januari 8.
“Maisha yake sasa yalikuwa yanasaidiwa na mashine. Baada ya pambano kali la ICU Simba alipaa mbinguni asubuhi ya saa 08:01:2025 saa 7:00 asubuhi na sekunde 43 mbele ya Mama, Baba na wajomba zake na Shangazi zake. Umekuwa mwanzo wa mwaka wa huzuni kwa familia yetu na tunashukuru kwa msaada wako na maombi,” aliongeza kwa majonzi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!