MSANII MAARUFU kutoka nchini Tanzania, Omary Mwanga maarufu kama Marioo amewashangaza wengi baada ya kukiri waziwazi kwamba hana ufahamu maana ya neno CEO kwa urefu.
Msanii huyo alifunguka haya wakati wa mazungumzo na mshawishi mmoja wa mitandaoni katika video moja ambayo imevutia hisia na maoni mseto mitandaoni.
Mtu huyo alimtaka kubainisha maana ya neno CEO ikizingatiwa kwamba yeye ndiye CEO wa lebo mpya ya Badnation, lakini Marioo akasema kwamba anajua tu ni mtu mkubwa lakini kirefu chake wala hajui.
“CEO kirefu chake? Aah, mimi sijui lakini naamini ni kiongozi yaani. Mimi hapa ndio CEO lakini ukweli sijui kirefu chake maana sijasoma mimi sasa nijulie wapi,” Marioo alijibu huku akisisitiza kutambuliwa tu kama CEO wa Badnation.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya ya Nairobi kutoka kwa albamu yake, ngoma ambayo alimshirikisha mkali wa hizo shughuli kutoka nchini Kenya, Bien.
Lebo yake ya Badnation kwa sasa inajivunia kuwa na wasanii wawili, yeye na msanii wake aliyemtambulisha mwaka jana kwa jina Stans Ooh.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!