RAPA STEVO Simple Boy amefunguka kwa undani kiini cha ziara yake ya takribani wiki moja nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka jana.


Akizungumza kwenye mahojiano na mwanablogu Trudy Kitui, Stevo Simple Boy alifichua kwamba ziara yake haikuwa ya kujivinjari bali ilikuwa ya kufuatilia miadi ya kikazi.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Msanii huyo aliyesafiri na meneja wake Machabe alisema kwamba alikuwa anafuatilia ahadi ya kolabo na moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri kutoka nchini humo, Harmonize.


Alisema kwamba alihisi Harmonize alivutiwa na ngoma yake ya ‘Inauma lakini itabidi umezoea’ aliyoifanya miaka ya nyumba baada ya kumuona bosi huyo wa lebo ya Konde Music Worldwide akiimba kipande chake.


Hivyo alifunga safari kufuatilia kama angeweza kufanikisha kolabo hiyo, jambo ambalo alisema kwa bahati mbaya halikufaulu.


“Tanzania nilikuwa nimeenda kutafuta Harmonize na Simba (Diamond Platnumz). Kwa bahati mbaya sikukutana na wao kwa sababu muda wetu na wao haukuoana. Lengo langu lilikuwa, kama naweza kurudisha nyumba kitambo kidogo, kuna wakati ile ngoma yangu ‘inauma but itabidi tuzoee’ Harmonize aliimba kipande kifupi…”


“…na wakati alikuwa hapa Kenya akapigia simu meneja wangu wa kitambo akisema angetaka kufanya kazi na mimi. Lakini vitu havikuenda sawa, hivyo nilikuwa nimeenda kumtafuta huko angalau tufanye hata kolabo moja. Kwa bahati mbaya hatukuweza kukutana lakini huu mwaka nafikiri itatimia,” Stevo alieleza.