MPENZI wa zamani wa Harmonize, Wolper Jackline amefichua kwamba ndoa yake na mumewe Rich Mitindo imesambaratika.


Wolper ametoa tangazo hilo kupitia kwa Instagram yake, ikiwa ni miaka miwili tu tangu walipofunga harusi yao kanisani mwishoni mwa mwaka 2022.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wolper aliweka wazi kwamba yeye na baba wa wanawe wawili, Rich Mitindo si mtu na mumewe tena, kwani wamefikia uamuzi wa kuachana na hawahitaji ushauri wowote, haswa kuhusu kurudiana.


Hellow Mashabiki zangu, marafiki wote mnao nitakia mema.Ni kwa masikitiko mengi sana mmekuwa mkinitumia message, links, na Clips mbalimbali, huku mkinishauri, kuniombea na kunitia moyo. Nimepokea msg zenu zote kwa moyo wa Shukrani sana. Na Mungu awabariki wote mnao nitakia mema, na hata wale wenye nia tofauti na njema pia mbarikiwe.

“Lakini naomba niwatoe wasiwasi na mashaka juu ya furaha na amani ya moyo wangu. Mimi na mzazi mwenzangu Rich (Baba P) hatupo pamoja (TUMEACHANA),”
Wolper alisema.


Aidha, mjasiramali huyo aliweka wazi kwamba hakuna njia yoyote ya kubadili msimamo wake kwani tayari yuko kwenye mchakato wa kuwasilisha talaka rasmi ya kutengana na Baba P, kama anavyomdekeza.


“Nipo kwenye process za Divorce/Talaka. Hivyo, mashauri yote na huruma juu ya mambo yanayo endelea na mzazi mwenzangu, msiyalete kwangu tena. Ni mtu ambae yupo huru kufanya chochote kinacho mpendeza.


Na hii niseme tu si kwa ubaya haijalishi mtalipokeaje wengine lakini maisha halisi ya ndoa yangu nayajua mimi na mwenzangu kwahiyo tutabaki kuheshimiana kama wazazi na kulea watoto wetu lakini swala la mahusiano ya ndoa hilo halipo!

Nawapenda sana nashukuru kwa msg zenu nyingi za kunitia moyo kutokana na mambo mnayoyaona huko lakini niwaambie tu mimi nipo sawa na muache kunihusisha na mambo yanayoendelea kwa mzazi mwenzangu kwasababu hayanihusu na nisingependa kuongelea hayo,”
Wolper alisema.


Harusi hiyo ilizungumziwa sana mitandaoni mwezi Novemba 2022 na Wolper ambaye wengi wanamjua kama Mama P alionesha kufurahishwa kwake kupitia Instagram yake.

"Huu wakati tu?❤️ Moyo wa shukurani ?Wapenzi hivi karibuni tunaingia mubashara @bona_tv." Wolper alinukuu picha zilizopigwa wakati wa harusi hiyo.

Wanandoa hao walimkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja, mtoto wa kiume, mwaka 2021.