MCHEKESHAJI maarufu kutoka nchini Nigeria, Mark Angel amefichua kwamba mwaka haujamuanzia vizuri kwani amejikuta katika dimbwi la hasara kubwa.
Mchekeshaji huyo alifichua taarifa hizo kupitia Instagram yake siku moja iliyopita ambapo alihadithia jinsi alitapeliwa zaidi ya dola milioni 3 na walaghai waliojifanya kuwa wafanyibiashara wa ubadilishanaji wa fedha.
Mark Angel alisema kwamba alijikuta katika mikono ya walaghai hao ambao walimkwapua zaidi ya shilingi za Kenya, milioni 478 na sasa yuko katika shimo la madeni mengi.
“Mwaka wa 2024 ulianza kama kila mwaka mwingine, lakini sikujua ni kiasi gani ungenijaribu ni kiasi gani ungenivunja, lakini mwishowe utanibadilisha. Ilikuwa mwaka nilipoteza kila kitu. Niliamini mikono mibaya katika forex na nikapoteza pesa zangu zote.”
“Hakuna mtu aliyejua isipokuwa familia yangu na mduara wa karibu zaidi. Uzito wa hasara hiyo, zaidi ya dola milioni 3.7 za fedha za wawekezaji zilikuwa za kutosha. Karibu kunipeleka gerezani; imenizamisha katika madeni,” Mark Angel alisema.
Aidha, mchekeshaji huyo alieleza kwamba hakuweza kusaidia chochote kwani alitazama kwa huruma mali yake yote yakitwaliwa na wenye waliokuwa wanamdai.
“Na moja baada ya nyingine, nilitazama mali zangu zote zikiingia mikononi mwa wakopaji. Ilionekana kana kwamba ulimwengu wangu ulikuwa ukiporomoka, na katika nyakati za giza sana, nilifikiria kumaliza yote,” alifunguka.
Mwanamume huyo alisema kwamba alifikiria kujitoa uhai lakini uwepo wa Mungu ukamjia wakati wa kiza kinene katika maisha yake.
Katika msukosuko huo, Mark Angel alisema kwamba alipata msaada wa kweli kutoka kwa mchungaji wake, marafiki zake wachache lakini pia mpenzi wake wa zamani.
“Lakini Mungu…Kama si kwa rehema Zake, nisingekuwa hapa nikiandika haya. Alituma malaika maishani mwangu wakati nilipowahitaji zaidi. Baraka, rafiki yangu ambaye alikuja kuwa familia, hakukata tamaa juu yangu. Mchungaji wangu na mke wake walisimama karibu nami, wakiniombea na kuniongoza. Binti zangu, Victoria na Mila, walinikumbusha uzuri wa maisha, hata yalipokuwa magumu. Mke wangu wa zamani Mandy alinyoosha mkono wa wema ambao sitausahau,” alisimulia.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!