JAMAA MMOJA katika mtandao wa X amewashangaza wengi baada ya kusimulia kisa cha kijana mmoja wa miaka 19 ambaye alimuibia bosi na ambaye ni mwalimu wake wa masomo ya nyanjani katika kipindi cha miaka 2.
Kwa mujibu wa simulizi hilo, kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alitumika kipindi cha miaka 2 na mwalimu wake wa mafunzo ya nyanjani akimuibia kiasi kidogo kidogo cha hela na kuzitumia bila bosi kujua.
Baada ya kukamatwa, ilibainika kwamba kijana huyo alikuwa ameiba zaidi ya shilingi milioni 2 kutoka kwa bosi wake huku akizitumia kwa njia mbalimbali, ikiwemo kucheza Kamari.
“Mvulana mwenye umri wa miaka 19 ambaye alikuwa akipitia programu ya uanafunzi alikuwa akiiba pesa kutoka kwa bosi wake. Katika muda wa chini ya miaka 2 akiwa na bosi wake, alikuwa ametuma zaidi ya 750k kwa wazazi wake, 500k kwa mpenzi wake, 420k za kamari, 700k kwa mambo ya kipuuzi, na zaidi ya milioni 1.7 katika akaunti ya akiba,” jamaa huyo alieleza.
Aidha, alielekea mbele kuwanyooshea wazazi kidole cha lawama, akisema kuwa kutoka kwa uthibitisho wa mazungumzo ya kijana huyo na wazazi wake kwa njia ya simu, wazazi ndio walikuwa wanampa shinikizo la kuwatumia pesa.
“Kutokana na mazungumzo yake ya simu, wazazi wake walikuwa wakidai pesa hizi kutoka kwake. Baadhi ya wazazi ni wawezeshaji wa uharibifu huu katika jamii yetu. Ndio maana mvulana wa miaka 20 ambaye hajui chanzo cha mapato angerudi nyumbani na Benz, na wazazi wangekuwa wakicheza kwa ajili yake. Tumemlaumu rais vya kutosha. Wacha tuanze kutazama kioo,” jamaa huyo alimaliza.
Tazama chapisho hilo hapa jinsi watu walichangia maoni yao kuhusu kisa hicho;
https://x.com/CaptainArinze/status/1875632901389427053
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!