Mchoraji katuni mashuhuri Gideon Kibet almaarufu Kibet Bull alithibitisha kuachiliwa kwake Jumatatu jioni na kuweka wazi kuwa yuko salama na yuko sawa.
"Nilikuwa nataka nithibitishie Wakenya kwamba niko salama na nimefika nyumbani salama," Kibet Bull alisema.
“Mbeleni sikuwa najua niko wapi. Kidogo kidogo nilienda mbele niko Luanda, hapo Luanda nikatafuta mahali pa kukaa juu ya usalama mpaka ifike asubuhi ili nisafiri nyumbani. Niliachiliwa kitu saa tisa hadi saa kumi asubuhi,” niliongea.
Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Egerton pia alifichua kuwa yuko vizuri kiafya na hana majeraha yoyote mwilini mwake baada ya kukaa siku nyingi na watekaji nyara wake. Pia alithibitisha kuwa kaka yake ambaye pia alidaiwa kutekwa nyara yuko sawa pia.
Kibet alitoa shukurani zake kwa wanamtandao wote walioshinikiza kuachiliwa kwao na kuendelea kuikosoa serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa ikiwashughulikia wakosoaji.
“Kutekwa nyara kupo, naweza kuthibitisha hilo. Mimi naomba serikali kuwa na uhuru wa kuongea ama watumie kutumia poa kama kupeleka mtu kortini,” alisema.
Kibet alisema atakuwa akisimulia zaidi kuhusu mambo yaliyojiri na mipango yake ijayo baada ya akili yake kutulia.
Mnamo Jumatatu, vijana wengine wawili ambao walidaiwa kutekwa nyara mnamo Desemba walipatikana wakiwa hai.
Hii iliongezeka hadi nne idadi ya wale walioachiliwa hadi sasa baada ya kudaiwa kutekwa nyara.
Familia za Billy Mwangi, Peter Muteti, Bernard Kavuli na Rony Kiplangat walisema jamaa zao walikuwa wamewasiliana nao.
Mwangi na Muteti walikuwa wamekutana na familia uso kwa uso..
Maafisa walisema Rony alipatikana katika Kaunti ya Machakos, na Bernard Kavuli, ambaye alitekwa nyara Ngong, alipatikana Kitale.
Walikuwa wakihangaika kufikia
familia zao.
Peter Muteti alipatikana Nairobi CBD, na walioshuhudia walisema alikuwa amechanganyikiwa na sasa anapata nafuu kutoka nyumbani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!