MSANII NA MJASIRIAMALI Esther Akoth Kokeyo maarufu kama Akotee ameahidi kutoa msaada wa kimasomo kwa watoto 4 mayatima ambao picha yao ya kutia huruma wakiwa kwenye jeneza la marehemu mzazi wao ilevutia hisia nyingi na nzito mitandaoni.
Watoto hao wadogo 4 walisimamishwa mbele ya jeneza la mzazi wao kwa picha ya mwisho ya kumbukumbu, na picha hiyo imevutia hisia nyingi na nzito miongoni mwa watumizi wa mitandao.
Hata hivyo, haijulikani hafla hiyo ya mazishi hayo ya kutia huruma ilifanyika wapi, lakini watu wengi wameomba msaada wa jinsi wanaweza fikia familia hiyo changa iliyoachwa.
Mmoja wa watu ambao wameomba kusaidiwa kufikia watoto hao ni Akothee ambaye ameahidi kuwapa msaada wa kimasomo watoto hao katika shule yake ya Akothee Foundation.
Msanii huyo aliomba mtu yeyote anayeweza kumpa msaada wa kuwafikia kujitokeza, akisema kuwa japo shule yake si ya bweni, lakini angeomba kuwasaidia mradi tu wawe na mtu angalau mmoja kutoka kwa uko atakayewatunza ili kufikia masomo kwa kutwa.
“Moyo wangu umeumizwa na kuona watoto hawa. Je, kuna yeyote aliye na habari kamili au maelezo kuhusu jinsi tunavyoweza kusaidia? Ingawa shule yangu bado si taasisi ya bweni, ikiwa wana mlezi au mwanafamilia aliyesalia, niko tayari kuwahifadhi chini ya uangalizi na mwongozo wa ndugu zao wa damu.”
“Nitatoa chakula, elimu, malazi, matibabu, na usaidizi mwingine wowote wa kimama wanaohitaji,” Akothee aliahidi.
“Walakini, ni muhimu kwamba waambatane na mtu wa familia. Ulimwengu unaweza kuwa wa kikatili sana, lakini kwa pamoja, tunaweza kuleta mabadiliko. Mungu akubariki mwaka huu kwa kugusa mioyo,” aliongeza mama huyo wa watoto 5.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!