KANISA moja la dhehebu la kiadiventista nchini Ghana limegonga vichwa vya Habari baada ya kuwatambua na kuwatuza wasichana takribani 20 kwa kutunza usichana wao licha ya kuwa katika umri wa baleghe.
Kanisa hilo la SDA lilifanya utambuzi huo mwishoni mwa juma ambapo liliwaita mbele ya madhabahu wasichana hao na kuwapa zawadi ya pesa taslimu kwa kuhifadhi ubikira wao.
Kwa mujibu wa habari, wasichana hao wenye umri wa kati ya miaka 13 na 16 walipokea kiasi cha fedha ambacho hakikutajwa kwa ajili ya kuwatunza wakati wa ibada ya Shukrani.
Naye Mratibu wa Shirika la Vijana Waadventista Wanawake Ministries, Wilaya ya Wenchi Magharibi, Bibi Nana Amponsah Poku aliwapongeza wasichana hao kwa kutunza ubikira wao huku akiwahimiza kuutunza hadi ndoa yao.
"Mungu alikuumba mrembo wa kipekee na hupaswi kuruhusu mtu yeyote akuvutie na kuvunja ubikira wako hadi uoe", aliwasihi wasichana hao na kuwataka wawe waangalifu kuhusu marafiki wanaotangamana nao mnamo 2025.
"Sherehe ya zamani ya Bragoro au Dipo ilikuwa muhimu sana katika kuhifadhi ubikira wa wasichana na kudhibiti mimba za utotoni ambazo ni hatari kwa ukuaji na maendeleo ya wasichana na wanawake," alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!