KENNEDY RAPUDO, mume tajiri wa mwanasosholaiti Amber Ray kwa mara nyingine tena amekanusha madai ya kuhusishwa na biashara haramu ya kutakatisha fedha na kughushi dhahabu.


Kupitia kwa taarifa ndefu kwenye ukurasa wake wa Instagram, Rapudo alisisiti9za kwamba biasara ya kutakatisha fedha na kuuza dhahabu bandia sio njia yake na wala haitokuja kutokea kuwa biashara yake.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Rapudo ambaye ni tajiri msiri kuhusu chanzo cha utajiri wake alisema kwamba wachache ambao wanamfahamu vizuri wanaweza toa ithibati kuwa utajiri wake ni halali.


“Utapeli wa dhahabu? Utakatisaji wa fedha? Hizo sio njia zangu na haziwezi kuwa njia zangu. Ukweli ni kwamba watu ambao wananijua kiukweli wanaelewa maadili na kanuni zangu. Sijawai jihusisha katika kitu chochote haramu,” Rapudo alithibitisha.


Rapudo alisema kuwa kama wale wanaofuatilia Habari za biashara hizo haramu wanataka kupata ukweli, basi wanaweza pata majibu kutoka kwa idara husika kama vile DCI.


Tajiri huyo alisema kwamba kwa vile aliamua kuweka maisha yake faraghani na kuficha vyanzo vya utajiri wake haimaanishi kwamba ni haramu.


“Kwa vile mtu aliamua kuishi maisha ya faragha na kutanika vyanzo vya utajiri wake haina maana kwamba wanajihusisha katika biashara haramu. Inasikitisha sana kuona jinsi watu wameamua kujikita katika kufuatilia mambo ya watu badala ya kuzingatia maisha yao.”


“Wakati wanaongea, nitaendelea kusonga mbele, kujenga maisha yangu kwa njia sahihi, njia moja ya kweli kwa kila hatua,” Rapudo aliongeza.


Rapudo alisema kuwa wakati alikuwa maskini miaka ya nyuma, hakuna ata mtu mmoja aliyefanya uthubutu wa kufuatilia chanzo cha utajiri wake, lakini sasa kwa vile anavyo, kila mtu yuko na uchu wa kutaka kujua.


“Hata hivyo, wakati nilikuwa maskini miaka ya nyuma, hakuna aliyethubutu kufuatilia chanzo cha umaskini wangu. Ama tuseme ni wivu, njaa na roho chafu?” alihoji.


Alisema kwamba kila mtu kwa sasa anafaa kuelekeza nguvu zake kwa kukosoa uongozi mbaya wa serikali na si katika kupoteza usingizi kwa utajiri wa mtu binafsi.