Mechi kubwa ya Ligi Kuu ya Uingereza kati ya klabu za Liverpool na Manchester United kwenye Uwanja wa Anfield iko shakani kuendelea Jumapili jioni.
Hii ni baada ya theluji kunyesha usiku kucha katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa Uingereza ambako kuna Uwanja wa Anfield unapatikana.
Katika taarifa yake Jumapili asubuhi, klabu ya soka ya Liverpool iliripoti kuwa kulikuwa na mkutano wa usalama kutathmini hali ya anga na hali ya usafiri.
Kundi la Ushauri wa Usalama la Halmashauri ya Jiji la Liverpool linatazamiwa kukutana tena saa sita mchana, saa za Uingereza (saa nane mchana saa za Afrika Mashariki), ili kutathmini hali hiyo baada ya mkutano asubuhi ya leo.
"Kikao cha usalama kilifanyika leo asubuhi kutathmini hali ya hewa na hali ya usafiri kwa mechi ya leo dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Anfield," Liverpool ilisema katika taarifa.
Katika taarifa hiyo, klabu hiyo ilieleza kuwa hadi kufikia Jumapili asubuhi, mechi bado imepangwa kuendelea na walitangaza mipango ya kuhakikisha mechi inaendelea vizuri.
"Katika hatua hii mechi imepangwa kuendelea kama kawaida na kila juhudi zinafanywa ili mchezo uendelee. Mkutano zaidi wa usalama utafanyika tena saa sita mchana ili kutathmini hali za hivi punde. Tutasasisha wafuasi haraka tuwezavyo,” ilisema taarifa hiyo.
Maeneo ya Merseyside na kaskazini-magharibi yalikuwa na dampo la theluji usiku kucha na hivyo kuathiri mechi ya Jumapili ya Liverpool dhidi ya Manchester United kwenye Anfield.
Mechi hiyo imepangwa kuanza saa kumi unusu alasiri kwa saa za Uingereza, na saa moja unusu jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Mashabiki watalazimika kusubiri kujua iwapo mechi hiyo itachezwa.
Mwezi uliopita mechi ya kwanza ya Merseyside kati ya Everton na Liverpool katika uwanja wa Goodison Park iliahirishwa kwa misingi ya usalama.
Katika tukio hilo upepo mkali kutoka Storm Darragh ulisababisha usumbufu mkubwa wa usafiri ndani na nje ya jiji.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!