Naibu Rais Kithure Kindiki amekanusha madai ya kuwepo mgawanyiko katika serikali ya Kenya Kwanza.

Akizunguma Jumamosi wakati wa hafla ya harusi ya mtoto wa Waziri wa Wanyamapori, Rebecca Miano, Peter na bi harusi wake Wambui, Kindiki aliwaomba Wakenya kumuunga mkono Rais katika Mwaka Mpya wa 2025 ili kusukuma nchi mbele.

Naibu rais alisema kwamba alikuwa amepewa likizo ya siku kadhaa na alikuwa amechukua mapumziko kutoka kazini.

"Nimebakia na masaa machache, likizo yangu inakaribia mwisho na kwa hivyo ninahitaji kufurahiya chochote kilichosalia. Puuza kila kitu kingine kabisa. Puuza kila kitu kingine. Usiingie kwenye mtego wa mambo madogo na madogo. Tuna biashara. Rais aliniruhusu siku chache za mapumziko,” Kindiki alisema.

"Ninahisi nina nguvu na ninaamini kuwa huu ndio mwaka ambao sisi sote tutamuunga mkono Rais na kuipeleka Kenya kwenye ngazi ya juu zaidi."

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Familia, marafiki na viongozi kadhaa wakiwemo Mawaziri na Makatibu Wakuu pia walikuwepo kwenye harusi hiyo ya Jumamosi.

Haya yanajiri siku kadhaa baada ya madai ya mgawanyiko katika serikali ya William Ruto kuibuliwa huku baadhi wakidai kwamba huenda rais na naibu wake walitofautiana.

Siku tatu zilizopita, Mkuu wa Uchumi wa Ubunifu na Miradi Maalum katika Afisi Kuu ya Rais, Denis Itumbi, alipuuzilia mbali tetesi za mtafaruku kati ya Rais William Ruto na naibu wake Kithure Kindiki.

Katika siku za awali, kulikuwa na uvumi kwamba viongozi hao wawili wanaoshikilia viti vya juu zaidi nchini huenda tayari wametofautiana.

Uvumi huo ulionekana kuenezwa zaidi baada ya naibu wa rais kukosekana kwenye mkutano wa mkesha wa Mwaka Mpya uliofanyika katika Kisii State Lodge usiku wa kuamkia Januari 1, 2025.

Katika taarifa yake siku ya Jumatano jioni, Itumbi alibainisha kuwa kinyume na madai hayo, rais na naibu wake wanashirikiana kikamilifu katika utekelezaji wa manifesto ya Kenya Kwanza.

“Rais na naibu wake wanashughulika kutekeleza MPANGO. Mwaka huu miradi na programu zitazungumza. Mnamo 2025, tutaonyesha UONGO kwa wakati halisi,” Itumbi alisema kupitia mitandao ya kijamii.

Mwanahabari huyo pia alitupilia mbali madai ya mabishano ya hivi majuzi kati ya DP Kindiki na msaidizi wa Rais Ruto Farouk Kibet.

“Ati DP @KindikiKithure alipigwa kofi na Farouk. UWONGO. Ati kuna mtafaruku, tafadhali andika UWONGO, hiyo inadumu,” alisema.

Jioni ya Desemba 31, 2024, naibu wa rais Kithure Kindiki hakuonekana mahali popote kwenye kikao cha chakula cha jioni cha mkesha wa Mwaka Mpya kilichofanyika Kisii State Lodge. Hili sio la kawaida na lilizua tetesi za mzozo kati ya watendaji wakuu huku Wakenya hata wakikisia ulikoanzia.