Watu tisa walifariki katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika barabara ya Kitale-Eldoret Ijumaa asubuhi.

 

Watoto watatu walinusurika wakiwa na majeraha.

 

Kamanda wa polisi kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi anasema ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa lori kushindwa kulimudu na kugonga matatu.

 

"Matatu hiyo ilikuwa na abiria 12 na ni watoto watatu pekee walionusurika," Mwanthi alisema.

 

Anasema polisi wanachunguza chanzo cha ajali hiyo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

 

Mwanthi alisema ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa moja asubuhi.

 

"Tunawatahadharisha watu wetu kuwa waangalifu barabarani na kuepuka mwendo wa kasi," alisema Mwanthi

 

Magari hayo yaligongana uso kwa uso na athari kubwa iliyowaacha baadhi ya abiria wamekwama kwenye mabaki ya matatu hiyo.

 

Matatu hiyo ilikuwa ikielekea Eldoret wakati lori hilo likielekea Kitale na walioshuhudia walisema magari hayo yaligongana kwenye sehemu nyembamba ya barabara mara tu baada ya soko la Soy.