KLABU ya Mamelodi Sundowns nchini Afrika Kusini wametoa tyaarifa ya kina kuhusu skendo kubwa ambayo imeripotiwa katika timu ya wanawake ya klabu hiyo.


Mamelodi Sundowns wamearifu umma kuhusu hatua iliyochukuliwa ya kumsimamisha kazi kocha wa timu ya wanawake Jerry Tshabalala kwa madai ya kuwauliza wachezaji maswali ya nguoni.


Kocha huyo mwanamume wa miaka 44 anaarifiwa kuwahoji wachezaji wake wa kike kuhusu ni mara ngapi wananyoa sehemu za siri na jinsi zinavyoonekana au maumbile yazo.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Mzee huyo wa miaka 44 inasemekana, miongoni mwa tuhuma nyingine nzito, amekuwa akitoa maneno ya ngono kwa wachezaji na wafanyakazi wa kike, akiwauliza ni mara ngapi wananyoa sehemu zao za siri na jinsi sehemu zao za siri zinavyoonekana au umbo," ripoti ya SABC Sport ilinukuliwa na GOAL.com Afrika.


"Pia anatuhumiwa kuingia wakati wachezaji wanabadilisha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kukataa kutoka kwenye chumba cha kubadilishia nguo, hata wachezaji wakiwa uchi kabisa."


Kupitia X, Mamelodi Sundowns wametangaza kuanzishwa kwa uchunguzi wa kina kuhusu madai hayo na kuahidi kuwa hatua zifaazo kisheria zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.


“Bodi ya Mamelodi Sundowns imefahamishwa kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu ambazo zimekuwa zikitolewa na wachezaji mbalimbali wa kike dhidi ya Kocha wa Timu yake ya Wanawake, Jerry Tshabalala.


Mamelodi Sundowns inaziona tuhuma hizi kwa uzito mkubwa na imeteua kampuni ya juu ya mawakili, Bowmans, kuchunguza madai haya na kuripoti kwa Bodi haraka iwezekanavyo.


Sundowns, kwa muda, imemweka Kocha Jerry Tshabalala likizo maalum kusubiri matokeo ya uchunguzi. Hili halifanyiki ili kutanguliza matokeo ya uchunguzi, bali kuhakikisha kwamba uchunguzi unaweza kuendelea kwa haraka na kulinda haki za wahusika wote.


Iwapo uchunguzi utabaini ukweli unaothibitisha hatua kuchukuliwa, Bodi itachukua mara moja hatua zinazofaa. Mamelodi Sundowns baada ya muda itatoa matangazo kuhusu matokeo ya uchunguzi huo na hatua zitakazochukuliwa,” Sundowns waliarifu kupitia X.


Onyesho bovu la Sundowns Ladies kwenye Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Caf mwezi Novemba linaweza kuwa dokezo kwamba huenda mambo hayakuwa sawa katika kambi yao.