MSANII Kevin Kioko
Bahati amekuwa na wiki isiyo ya furaha baada ya kufiwa na mamake wa kambo
aliyezikwa Jumamosi, siku moja tu kuelekea siku ya kuzaliwa ya msanii huyo
kutoka Mathare, Nairobi.
Bahati alifichua taarifa za kuzikwa kwa mama yake wa kambo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alishiriki msururu wa picha na video kutoka kwa hafla hiyo ya mazishi.
Alimuomboleza kama mwanamke ambaye baba yake alimpenda wa mwisho kabla ya kifo chake miaka kadhaa iliyopita.
“Imekuwa ni siku mbaya. Bado siamini kwamba umeenda. Ilikuwa ni kwaheri ya majonzi kwa mwanamke ambaye babangu alimpenda wa mwisho. Mama yetu amekwenda kuwa na Mungu. Salimia baba Bahati, tutaonana baadae,” Bahati aliandika.
Msanii huyo alimzika mamake wa kambo siku moja tu kabla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na haijulikana iwapo atasherehekea siku hiyo.
Kifo cha mamake wa kambo kinajiri wakati ambapo pia TikToker, Rachael Otuoma anaomboleza kifo cha mpenzi wake, mwanasoka Ezekiel Otuoma aliyefariki wakati Rachael anasherehekea siku yake ya kuzaliwa pia.
Otuoma alifariki baada ya vita vya muda mrefu na ugonjwa wa kupooza neva mwilini tangu mwaka 2020.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!