MSANII na mjasiriamali Esther Akoth maarufu kama Akothee amechagua kumsherehekea tiktoker Rachael Otuoma kwa upendo wa kipekee aliomuonyesha marehemu mumewe Ezekiel Otuoma hadi kifo chake.


Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Akothee aliwakosoa baadhi ya watu ambao walianza kuandika jumbe za kuhoji jinsi Otuoma alipata kifo chake wakati mkewe akiwa kwenye tafrija ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.


Akothee alihisi hoja kama hizo ni za kumkosea heshima Rachael, haswa kipindi hiki aqnapoomboleza, akiwataka watuy kuangalia zaidi kwa yale mazuri ambayo amemfanyia mumewe kwa miaka 4 aliyougua.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Mitandao ya kijamii imeunda jukwaa ambapo mtu yeyote anaweza kuchapisha chochote, mara nyingi bila huruma au akili ya kihisia. Uzembe na kutojali unaoonyeshwa na baadhi ya watu, hata wakati wa huzuni, unaweza kuwa mwingi. Watu wanaonekana kushindana juu ya kila kitu, hata katika kifo, na kusahau ubinadamu unaotufunga sisi sote,” Akothee alifoka.


Alisema yeye ameamua kumpa maua mrembo Rachael kwa kudhihirisha bayana kwamba kauli ya “katika ugonjwa na katika afya hadi kifo kitutenganishe” inawezekana.


“Katikati ya machafuko haya, ninataka kutambua na kuheshimu nguvu na uthabiti wa Rachel Otuoma. Mwanamke huyu wa ajabu anatoa mfano wa maana halisi ya "katika ugonjwa na afya, mpaka kifo kitakapotutenganisha." Kusimama kando ya mume wake katika nyakati za hatari zaidi kulihitaji nguvu nyingi za kihisia, kisaikolojia na kiakili. Wachache wangekuwa na ujasiri wa kufanya kile alichofanya, kujali bila ubinafsi na kwa upendo,” Akothee alimsifia Rachael.


Alisema kwamba mambo ambayo Rachael alikuwa akimfanyia Otuoma, japo madogo na ya kawaida yalikuwa ndio furaha na faraja kubwa kwa marehemu.


“Raheli, kujitolea kwako bila kuyumba ni ushuhuda wa nguvu ya upendo. Kila nilipokuona unamchezea mumeo, niliona furaha na faraja iliyomletea, unaweza usijue lakini unaongeza pumzi yake kwa tabasamu hilo,” alisema.


“Kwa wale wanaokosoa na kuhukumu, kumbuka kuwa huzuni ni ya mtu binafsi, na heshima ni sifa ambayo sisi sote tunapaswa kuidumisha. Raheli, jifariji kwa kujua kwamba ulitoa bora yako na kuheshimu nadhiri zako kwa ukamilifu,” Akothee aliongeza.