TIKTOKER Rachael Otuoma ameonyesha kuvunjika moyo vipande vuipande baada ya mumewe Ezekiel Otuoma kufariki dunia.


Rachael alithibitisha taarifa hizi kupitia ukurasa wake wa TikTok ambayo alifichua kwamba Otuoma alifariki wakati Rachael aqkifanya maandalizi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kufanyika.


Rachael ambaye amekuwa wa msaada mkubwa kwa Otuoma tangu 2020 alipopatikana na ugonjwa wa kufifisha neva mwilini, alitaja kifo cha mpenzi wake kama pigo lisiloweza sahaulika.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Kwa Mume wangu??Umeacha shimo moyoni mwangu ambalo hakuna mtu mwingine awezaye kulijaza Japo ilikuwa hivi karibuni sana?thats really broke my heart ? uliondoka kwenye birthday yangu ?haitakuwa sawa tena nilikupenda sana katika kifo nakupenda bado moyoni mwangu unashikilia nafasi ambayo wewe pekee unaweza kuijaza???Ilinivunja moyo wangu kukufungua lakini hukuenda peke yako, umeenda na sehemu yangu pia????????MPAKA MIMI TUKUTANE TENA,” Rachael aliandika kwa kuomboleza.


Ezekiel Otuoma amepumzika baada ya vita vya muda mrefu na Motor Neuron Disease. Motor neurone ugonjwa ni hali ambayo huathiri neva, husababisha udhaifu katika misuli, na kusababisha hatimaye kupooza.


Aligunduliwa na ugonjwa huo mnamo 2020.

Otuoma alichezea Ushuru Fc,Fc Talanta, AFC Leopards, Western Stima, Ulinzi Stars na Muhoroni Youth kabla ya kuachana na soka kutokana na hali yake ya kiafya.