WAZIRI wa zamani wa jinsia, utamaduni, sanaa na torati za taifa, Aisha Jumwa alizua vichekesho Ijumaa wakati alihudhuria hafla ya seneta wa kaunti ya Tana River, Danson Mungatana.


Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo naibu wa rais Kithure Kindiki na waziri wa madini na uchumi wa baharini Ali Hassan Joho.


Viuongozi wengi waliosimama na kuzungumza walisimulia jinsi walikuja kujuana na Mungatana na ilipofika zamu ya Jumwa, aliwachekesha wengi alipotania kwamba hajui mbona Mungatana hakumuona wakati wakiwa wadogo licha ya urembo wake.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Jumwa alitania kwamba akiwa binti mdogo alikuwa mrembo sana, akisema kwamba sasa hivi kidogo urembo umepunguka, na kuhoji kwa nini Mungatana hakuona urembo wake uliopitiliza na pengine kumuoa.


“Mimi ninafanana na babangu sana, na wakati huo babangu alikuwa ni mtu wa mambo mambo kiasi, hivyo wakili wake akawa ni mheshimiwa Mungatana. Mimi nilimjua Mungatana kama wakili wa babangu nikiwa msichana mdogo mrembo, si sasa hivi mambo yameisha lakini sijui kwa nini Mungatana hakuniona wakati huo,” Aisha Jumwa alitania huku watu wakijiachilia kwa vicheko.


Hata hivyo, waziri huyo wa zamani alishukuru jinsi hatima ilikuja kufanya maisha yao baadae, akifichua kwamba sasa hivi Mungatana ni shemeji yake.


“Lakini hata hivyo nashukuru kwa sababu Mungatana sasa ni shemeji yangu nan iko na raha sana,” Jumwa alimaliza utani wake.


Seneta Mungatana aliandaa hafla hiyo ya shukrani na kurudi nyumbani kwake katika kijiji chake cha Ngao kaunti ya Tana River, hafla ambayo iliwavutia hadi spika wa seneti, Amason Kingi.