MBUNGE wa Kapseret,
Oscar Kipchumba Sudi ameonyesha furaha yake baada ya chuo kimoja cha kibinafsi
kutambua mchango wake katika uongozi na kumtunuku shahada ya uzamivu katika
uongozi na usimamizi.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Oscar Sudi alirundika picha akiwa amevalia joho la mahafali katika chuo hicho na kufichua kwamba alitunukiwa shahada ya kiheshima katika uongozi.
Alishukuru chuo hicho kwa kutambua mchango wake katika uongozi na usimamizi na pia kuchukua nafasi hiyo kuwahongera mahafali wenzake kwa juhudi zao kulipa siku ya kufuzu kwao katika chuo anuwai cha Eldoret.
“Nina heshima kubwa kupokea Shahada ya Heshima ya Uzamivu katika Uongozi, Utawala, na Usimamizi kutoka Chuo Kikuu cha Kikristo cha Northwestern katika The Eldoret National Polytechnic. Utambuzi huu unasisitiza asili isiyo na kikomo ya elimu-kweli haina mipaka. Kwa wahitimu wa mwaka huu, pongezi kwa hatua hii ya ajabu. Safari zako za mbele ziwe na athari na za kutia moyo,” Sudi alichapisha.
Mashabiki wa mbunge huyo mtetezi mkali wa sera za serikali ya siku walifurika kwenye maoni na kumpa hongera za dhati kwa juhudi zake zilizotambulika na kutuzwa.
Haya hapa baadhi ya maoni;
Sialo Kimiring: “Hongera kwa utambulisho huu unaostahili! Mafanikio yako yanaangazia uongozi wako na kujitolea kwako. Nakutakia athari na msukumo unaoendelea katika juhudi zako zote!”
Alvin Njoroge: “Hongera. Unanitia moyo sana na hadithi yako ya maisha, Mungu akubariki, Siku moja tutakutana.”
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!