MJASIRIAMALI Simon Kabu amewapa mashabiki wake moja ya kumbukumbu za kipekee jinsi kampuni ya familia yake, Bonfire Adventures ilivyozaliwa.


Kupitia ukurasa wake wa Facerbook, Kabu amedakia #TBT, leo ikiwa ni Alhamisi siku ya watu kuonyesha kumbukumbu zao za zamani, nzuri na mbaya.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kwa upande wa mfanyibiashara huyo, alichagua kusherehekea siku kampuni yake ya Bonfire Adventures ilipozaliwa mwaka wa 2007.


Katika picha hizo, Simon na Sarah – wakiwa wadogo kiumri wanaonekana wakifanya mazungumzo kwa tabasamu pana nyusoni mwao.


Kabu alifichua kwamba siku hiyo ndio Bonfire Adventures ilipozaliwa wakiwa katika hafla ya kitalii huko Lukenya.


“TBT, Tarehe moja Desemba mwaka 2007, siku Bonfire Adventures ilipozaliwa kutoka kwa kundi la vijana wadogo wataalamu. Tukiwa katika hafla ya pamoja huko Lukenya,” Simon Kabu aliandika.


Kabu anaibua kumbukumbu hii wakati ambapo kuna uwazi wa kukosekana kwa maelewano baina yake na mkewe, ambaye pia ni mwanzilishi mwenza wa kampuni hiyo ya kitalii.


Sarah aliweka wazi kupitia msururu wa jumbe kwenye mitandao ya kijamii akisisitiza kwamba hatotaka tena kuhusishwa na jina la Kabu huku akikumbatia jina jipya ‘Sarah Mtalii’.


Ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu mfarakano wao kuenea mitandaoni, wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza wiki moja iliyopita katika hafla ya kufunga mwaka ya kampuni hiyo.


Katika hafla hiyo, Sarah na Simon walioonekana kuwa na ugumu katika kukata keki ya pamoja jambo ambalo lilizua mjadala pevu katika mitandao ya kijamii.