KIZAAZAA kilishuhudiwa katika kanisa moja wakati wa hafla ya harusi.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika tukio hilo ambalo limezua maoni kinzani kwenye mitandao ya kijamii, bibi harusi alionekana amejiremba vikali tayari kwa siku yake ya ndovu kumla mwanawe, lakini mchungaji wa kufungisha harusi yake alionekana kutofurahishwa na urembo wake.


Mchungaji aliamuru mara moja kwa bibi harusi kujifuta urembo wake wote aliokuwa amejuipodoa haswa usoni ili kuonyesha sura yake halisi kabla ya kufungisha harusi yake.


Tukio hilo lilishirikiwa kwenye jukwaa la blogu ndogo, X na mwana mtandao aliyetambulika kama @teeniiola.


Kulingana na ripoti hiyo, kanisa ambalo halivumilii make up, lilimtaka bibi harusi aitoe baada ya kufanya hivyo kwa ajili ya hafla hiyo.


Video iliyoshirikiwa inamuonyesha bibi harusi akiwa amekaa huku marafiki zake wakisafisha vipodozi, na kuondoa kope alizokuwa amebandika.



@teeniola aliandika…


"Kanisa lilimwomba bibi harusi kuondoa vipodozi vyake siku ya harusi yake ?‍️"


Tukio hilo lilizua mjadala baadhi wakimsuta mchungaji kwa kuharibu siku ya maharusi na wengine wakimuunga mkono kwa kuwataka maharusi kuwa halisi na si kuvalia nyuso za kuigizia urembo na utanashati.


Haya hapa baadhi ya maoni;


@queenlizzie61 alisema: "Unajua mambo haya, isipokuwa haukuhudhuria darasa la ndoa na ushauri"


@emryskixxy alitoa maoni: “Kwa nini?


@Tooshugary4U alitoa maoni: "Faida ambayo pls, nitahamia kanisa la karibu mara moja!"


@queenlizzie61 aliandika: “Isipokuwa wewe pia ulipiga picha kabla ya kwenda kanisani. Kwa hivyo sinema hii yote sio lazima"


@gold_06768 alitoa maoni yake: "Ila labda kanisa halikubali vipodozi"


@Olaferanmijulo aliandika: “Msisome mwongozo wa kanisa kwa ajili ya harusi ni ???”


@MORRENICS alisisitiza: "Anafahamu hilo, anataka tu kujiaibisha"