CROSS-DRESSER Kelvin Kinuthia amewasuta wanawake ambao wanatangaza kuwahudumia wanaume wao katika nyumba zao.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, KInuthia alionekana kuwakashifu wanawake ambao wanafanyia wanaume wao kila kitu na kisha kuenda kutangazia umma kwamba wanafadhili maisha ya wanaume wao.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kinuthia alifichua kwamba wengi wanaotangaza hivyo aghalabu huw wanafadhili maisha ya mwanamume mmoja tu lakini akasema kwamba yeye ameweka ijana hadi 16 na hajawahi zungumza hilo kwa umma.


“Huku nje mnaweka mwanamume mmoja tu na mnaenda kutangaza kwa runinga, mimi ambaye nimeweka vijana 16 nafaa kuongea wapi?” Kinuthia alihoji.


Kauli yake inajiri siku chache tu baada ya mkuza maudhui Alma Mutheu kuzua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii alipomvua nguo hadharani mpenzi wake Gift Muziq kwamba anakula kwa mgongo wake.


Mutheu alifichua hayo wakati wa mahojiano ya kipekee na Oga Obinna, ambapo alisema kuwa yeye ndiye anafadhili maisha mazuri ya mpenzi wake.


“Inafika hatua mwanamke unachoka kufanya kila kitu, ni sawa, sio kila mtu ana uwezo, lakini huwezi kukaa na mtu muda mrefu sana, tuseme miaka mitatu au miwili. bado wanatoa kila kitu kama mwanamke hata kama ni kutoa nusu, hiyo ni kutoa," alisema.


"Nilishawahi kukutana na watu wengi sana waliniambia niachane naye, lakini kwa sababu nilikuwa nampenda, hakuna aliyeweza kuniambia chochote. Nilikuwa kama nitampa muda wa kuhangaika. Lakini imefika wakati bado anahangaika," aliongeza.


Suala hilo lilivutia hisia kinzani, baadhi wakisema kwamba mrembo huyo alifanya vibaya kuanika madhaifu ya mpenzi wake kwa umma.


Gift kwa upande wake alisema kwamba aliamua kupaka nywele yake rangi ya pink kwa sababu mpenzi wake anapenda hiyo rangi.


Akionekana kuchokonoa hilo, Knuthia naye alisema kwamba anatafuta mpenzi mwenye  atakuwa tayari kupata nywele rangi aipendayo yeye, akifichua kuwa rangi yake pendwa ni nyekundu.


“Hata mimi sasa hivi natafuta mwenye atapaka nywele rangi yangu pendwa, na mjue ni nyekundu,” Kinuthia alisema.