CHUO kikuu cha Kisii kimeonesha fahari yake katika uendelevu baada ya kuongeza msafara wa magari mengine mapya katika orodha ya magari yanayomilikiwa na chuo hicho.


Kupitia ukurasa wao wa Facebook, Chuo hicho kilitaarifu umma kwamba wamefanikiwa kununua ambulensi mpya ya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia jamii ya chuo hicho.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kando na ambulensi, chuo hicho pia kilionesha picha za mabasi mawili mapya yenye uwezo wa kubeba abiria 67 kila moja.


“Kwa furaha, shauku na furaha isiyoisha, familia ya Chuo Kikuu cha Kisii leo imekaribisha Ambulansi ya kisasa, ya kitaalamu na iliyo na vifaa vya kutosha pamoja na mabasi mawili ya kubeba watu 67 kila moja,” uongozi wa chuo ulisema.


Wakitetea hatua hiyo, chuo hicho kilisema kwamba hii ni moja ya mkakati wa kuboresha huduma kwa jamii nzima ya chuo hicho.


 “Nyongeza 3 ni uamuzi wa kimkakati unaokaribishwa sana na Baraza la Chuo Kikuu na utasaidia sana katika kuhakikisha utendakazi katika Chuo Kikuu unakuwa bora zaidi,” waliongeza.


Wakati akiwaalika, Mwenyekiti wa Baraza alifurahishwa na maendeleo ya ajabu ya Chuo Kikuu cha Kisii.


Chuo kikuu cha Kisii ni miuongoni mwa vyuo vichache ambavyo vinaonyesha maendeleo makubwa wakati ambapo idadi kubwa ya vyuo vikuu vya serikali vinapitia changamoto za kifedha.


Vyuo vikuu kama Moi na Nairobi vimekuwa katika wakati mgumu miaka ya hivi karibuni kutokana na kile kinachokisiwa kuwa ni kutokuwa na hela za kutosha kuendeleza shuli vyuoni humo.