MCHEKESHAJI na mchungaji
wa kanisa la JCM, Muthee Kiengei amevunja kimya chake baada ya taarifa kuibuka
kwamba mchungaji wa kanisa lake tawi la Mtwapa amefariki.
Taarifa za awali ambazo zilithibitishwa na Kiengei kwenye chapisho lake zilifichua kwamba mchungaji huyo alifariki kwa kujitoa uhai.
Kiengei alimuomboleza kwa ujumbe wa dhati akisema kwamba japo amekwishatangulia mbele za haki, lakini uamuzi aliouchukua ni mbaya kwani yeye kama mchungaji wake mkuu angemsikiliza kama angemfuata kuzungumza.
“Hata kama ungekuwa mwisho wako, Kupambana nayo juu, Mtu angeweza kukusikia...... Nafsi ya kijana imeondoka, ikiahidi katika kofia ya utumishi na roho angavu,” Kiengei aliomboleza.
Pasta Kingei alifichua kwamba pasta huyo wa tawi la Mtwapa alisafiri hadi katika shamba lake la Sagana kaunti ya Nyeri alipojimalizia.
“Nilipopokea simu kutoka kwa mkeo, nilifikiri uko mahali fulani unaomba au labda unamtembelea rafiki na kukuta kwamba umemaliza maisha yako siku kadhaa zilizopita, mwili wako usio na uhai ukiwa umelala kwenye shamba la baba yako huko sagana....”
“Kwanini utoke Mombasa, Kukatisha maisha yako ya ujana??? How i hope ulizungumza na mtu..... Ipo siku Unyogovu pia utashuka moyo. Rest well bro Pst Peterson Mwangi of Jcm Church Mtwapa Mombasa,” Kiengei aliongeza katika ombolezo lake.
Hata hivyo, chanzo cha mchungaji huyo kijana kujitoa uhai hakijabainika, ikiwa imesalia tu kwamba ni unyongovu.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!