MFANYIBIASHARA wa kuuza samani, Gibson Murage Gitonga amesalia katika makadirio ya hasara kubwa baada ya moja ya duka lake kuteketea.

Katika picha na video zilizosambaa mtsndaoni mapema Jumatano, moja ya duka lake la fenicha lililoko Ruiru kaunti ya Kiambu lilishika moto.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Chanzo kiliarifu kwamba moto huo ulizuka alfajiri ya Jumatano na kiini chake kingali bad hakijabainika.


Hata hivyo, maafisa wa zimamoto waliwahi na kufanya juhudi za kuzima moto huo.


Muasisi huyo wa Modern Furniture Pacific alionekana akiwa amejishika tama akiangalia pasi na kuamini jinsi mtaji wake ulikuwa umemezwa na moshi mkubwa.


Wakenya kwenye mitandao ya kijamii waliguswa na taswira hiyo na kumfariji Murage kwa hasara hiyo kubwa.


Murage, aliyekuwa mchuuzi wa nguo za mtumba, alijitosa katika biashara ya samani huko Nyeri na kujipatia utajiri. Akiwa kijana mwenye tamaa, alifungua matawi jijini Nairobi kwa fahari nyingi pia.


Upanuzi huo umemfanya kujitosa katika duka lake la hivi punde, lililo katika Kaunti ya Nakuru. Wakenya waliokuwa wakistaajabia maendeleo yake walikuwa na huzuni baada ya kuona bidii yake katika duka la Ruiru ikiteketea kwa moto.